Jeshi
la Polisi Kanda Maalum limeendelea na oparesheni zake kuwatafuta na kuwakamata
majambazi wote wanaofanya uhalifu wa kutumia silaha na uhalifu mwingine ili
sheria ichukue mkondo wake. Katika oparesheni hiyo yamekamatwa majambazi wawili
kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuitumia katika matukio ya
ujambazi.
Kabla ya
kukamatwa kwa bunduki hiyo watuhumiwa walikuwa wamepanga kufanya tukio la
ujambazi katika maduka ya MPESA na TIGO PESA yaliyopo maeneo ya Sinza Madukani.
Majambazi hao waliahirisha kufanya tukio baada ya kushtukia mtego wa
polisi.
Mnamo tarehe
10/09/2014 majambazi hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa kuwa
yamejipanga kufanya tukio la uhalifu maeneo ya YOMBO DOVYA na kisha kuweka
mtego katika nyumba ya ASIA D/O ALLY KASHINDE anayekadiriwa kuwa na umri wa
miaka 70 iliyopo maeneo ya Yombo Makangarawe (M) wa Kipolisi wa Temeke. Baada
ya kuwakamata majambazi hao walipekuliwa katika chumba wanacholala ndipo
ilipopatikana silaha aina ya SMG
yenye namba IC 5740 ikiwa na risasi 07 ndani ya magazine. Bunduki
hiyo imekatwa mtutu na kitako. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kuwezesha
kuwakamata wengine wanaoshirikiana katika genge hili la ujambazi.
Majina ya watuhumiwa
wa ujambazi waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
1.
KHAMIS
S/O AMBA, Miaka 40, Mkazi wa Yombo Makangarawe.
2.
OMAR
S/O KHAMIS, Miaka 43, Mkazi wa Masasi Nyasa Mtwara
No comments:
Post a Comment