Monday, September 15, 2014

KUKAMATWA KWA TIKETI BANDIA 424 ZA MECHI YA NGAO YA HISANI KATI YA YANGA NA AZAM




Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda linawashikilia na kuwahoji watu wawili kwa kosa la kupatikana na tiketi bandia za mchezo wa mpira wa miguu wa kuwania NGAO ya JAMII uliofanyika mwishoni mwa wiki hii kati ya timu za YANGA na AZAM zote za jijini Dar es Salaam.

Watu hao walikamatwa usiku wa tarehe 13/09/2014 maeneo ya Mission Quarter, mtaa wa Masasi, Kata ya Kariakoo (M) wa Kipolisi Ilala Dare es Salaam baada ya polisi kupata taarifa juu ya kuwepo watu hao eneo la tukio. Polisi waliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata BARAKA S/O MZEE, Miaka 34, Mkazi wa Magomeni na NASSIB S/O KULWA, Miaka 37, Mkazi wa Temeke Mwisho. Walipopekuliwa walikutwa na tiketi bandia za mchezo huo wa ngao ya hisani kati ya timu ya Yanga na Azam zote za jijini Dar es Salaam.

KUPATIKANA KWA SILAHA AINA YA PISTOL NA RISASI SITA (6)
Jeshi la Polisi limefanikiwa kupata silaha aina ya pistol glock yenye namba TZ CAR 10315 yenye magazine moja na risasi 6 baada ya genge la wahalifu kukurupushwa na Polisi walipokuwa wakipanga kufanya tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha huko maeneo ya Tegeta Msichoke kata ya Kunduchi wilaya ya Kipolisi Kawe.
Tukio hilo lilitokea tarehe 3/9/2014 baada ya majambazi kukimbia na kutelekeza begi baada ya kupekuliwa na polisi walikuta sina hiyo pamoja na vitu vingine kama jeki moja, shoka ndogo moja, mkasi mmoja wa kukatia waya, tindo moja ya kutobolea ukuta, kisu kimoja kidogo na saa ya mkononi.  Pia ilikamatwa pikipiki moja yenye namba T.412 CXV aina ya King Lion rangi nyekundu ambayo imeachwa na wahalifu hao.
HITIMISHO
Kwa kuwa ili uhalifu utokee ni lazima pawe na fursa zinazoshawishi kutendeka kwa uhalifu. Miongoni mwa mazingira rafiki kwa ajili ya kufanyika kwa matukio makubwa hasa ya unyang`anyi wa kutumia silaha au nguvu  ni uendeshaji wa shughuli za uuzaji wa vileo bila kuzingatia sheria, upigaji wa muziki kwa sauti ya juu wakati wa usiku bila kikomo na kuendesha shughuli za biashara usiku bila ya kuwa na mfumo mzuri wa ulinzi na usalama.
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es salaam inatoa wito kwa wananchi, wafanyabiashara, wanahabari na makundi mbalimbali kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa hali na mali sambamba na kutoa taarifa za mitandao ya uhalifu ili Jeshi la Polisi liweze  kujipanga vizuri kukabili vitendo vya kihalifu na kuifanya jamii ya Dar es salaam iweze kuishi bila hofu ya uhalifu.
Pia tunasisitiza wafanyabiashara kuheshimu masharti ya yaliyopo katika leseni za biashara zao sambamba na kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ya biashara.

No comments:

Post a Comment