*Rais Kikwete asema ametoa maagizo Hazina kupandisha mishahara, kupunguza kodi
*Walimu wamuita shemeji, wakumbusha
mishahara
*Awataka wawakilishi wa wafanyakazi kusema
yao, si ya wengine
Rais Jakaya Kikwete (kulia), akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi na wa Mkoa wa Dar es Salaam, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 'May Day'.
Baadhi ya wafanyakazi wakipunga bendera za Shirikisho la Wafanyakazi nchini Tanzania (TUCTA), Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho wa Siku ya Wafanyakazi Duniani 'May day'.
Rais Kikwete akiwasili kwenye jukwaa la Uwanja wa Uhuru tayari kwa mapokezi ya maandamano ya wafanyakazi kuadhimisha
Siku ya Wafanyakazi Duniani 'May day'.
Rais Kikwete akiwasili kwenye jukwaa la Uwanja wa Uhuru tayari kwa mapokezi ya maandamano ya wafanyakazi.
Rais Kikwete akisalimiana na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Wafanyakazi na wa Mkoa kwenye jukwaa la Uwanja wa Uhuru.
Rais Kikwete akiwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, wakizungumza jambo, mara baada ya kuketi kwenye jukwaa la Uwanja wa Uhuru.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya siku yao ya wafanyakazi jijini leo.
Bendi ya Polisi ikiongoza maandamano ya wafanyakazi katika kuadhimisha siku yao ya May Day.
Polisi wa kikosi cha Bendi wakitoa heshima zai mbele ya Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maandamano ya wafanyakazi katika kuadhimisha siku yao ya May Day, jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete akiwa tayari kupokea maandamano ya wafanyakazi katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani 'May day', Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo.
Na Mwandishi wetu
RAIS Jakaya Kikwete amewahakikishia wafanyakazi nchini kuwa anatarajia kupandisha kima cha chini cha mshahara ili alau kikidhi mahitaji muhimu.
RAIS Jakaya Kikwete amewahakikishia wafanyakazi nchini kuwa anatarajia kupandisha kima cha chini cha mshahara ili alau kikidhi mahitaji muhimu.
Pia amewawaambia wafanyakazi anafanya juhudi kubwa za kuboresha maslahi
ya watuhumishi wa umma huku akiweka wazi
hata akimaliza muda wake Rais ajaye atajali maslahi yao, hivyo wasiwe na hofu.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo Dar es Salaam leo wakati akitoa hotuba yake katika sherehe za siku ya wafanyakazi ,Mei
Mosi.
Akifafanua kuhusu mshahara kwa watumishi wa umma,Rais Kikwete alisema kuwa Bajeti ya fedha ya mwaka 2014/2015 kima cha chini kitapanda.
Alisema kuwa kulikuwa na mjadala mkali kuhusu kima cha mshahara lakini aliamua kutoa maagizo ya kuhakikisha kima cha
mshahara kinapandishwa licha ya mapato ya Serikali kutokuwa makubwa.
"Mwaka jana mshahara ulipanda kwa asilimia 41 na mwaka huu tutauongeza. Hivyo bajeti ya mwaka huu kutakuwa na
nyongeza mpya ya
mshahara,"alisema Rais Kikwete.
"Natambua umuhimu wa kupandisha
mshahara kwa wafanyakazi hivyo mwaka huu mshahara utapanda tena ili
angalau watumishi waweze kujikimu kimaisha,"alisisitiza.
Aliongeza kuwa mwaka 2005 kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kilikuwa sh. 65,000 kwa mwezi lakini sasa
hivi ni sh. 240,0000.
"Kwa hali iliyopo sasa nyongeza kubwa ya mshahara kwa mara moja itakuwa ngumu lakini naamini kwa namna uchumi wetu
unavyoimarika tutafika mahala pazuri,"alisema Rais Kikwete.
Alisisitiza inawezekana atakuwa ameondoka madarakani lakini Rais atakayefuata atajali maslahi ya wafanyakazi huku akifafanua
kuwa utawala wake umekuwa ukijali zaidi wafanyakazi.
Kuhusu mshahara kwa sekta binafsi, Rais Kikwete alisema amekuwa hafurahishwi na kima cha chini katika sekta hizo
hakimfurahishi kwani bado ni kidogo.
"Ni muhimu kwa sekta binafsi
kuangalia namna ya kuongeza kima cha chini kwa watumishi wake.Maana
kiwango wanachopewa sasa ni kidogo.
"Nimepata taarifa kuwa sekta binafsi
wengi wao hawazingati kiwango kinachotolewa na Serikali lakini tayari
nimetoa magizo kwa wasaidizi wangu kuhakikisha mishahara
inaongezeka,"alisema Rais Kikwete.
Alitoa mfano kuwa kuna siku
alitembelea moja ya kiwanda nchini (jina analo), ambapo pamoja na ukubwa
wa kiwanda lakini mishahara kwa wafanyakazi wake iko chini.
"Nilipofika pale nikaoneshwa
ukubwa wa kiwanda na maelezo mengi lakini wafanyakazi wakaanza kusema
afadhali umekuja Rais tusemee, maana tunalipwa mshahara mdogo.Nikauliza
wanalipwa kiasi gani kwa mwezi wanakaniambia sh. 48,000.Inasikitisha
kweli,"alisema Rais Kikwete.
Alisema kuwa tabia ya tajiri kumlalia mfanyakazi ili apate utajiri si jambo nzuri na atakapokutana na waajiri itanoga.
Kodi ya mapato Rais Kikwete alisema lengo la Serikali ni kuwa na kodi chini ya asilimia 9 kwa mwaka huu na ndio lengo la Serikali kuendelea kupunguza kodi kwa mfanyakazi.
Alisema kuwa awali kodi ilikuwa
asilimia 14.5 na ilishuka mpaka alimia 13 na hivi sasa imefikia asilimia
10.Hata hivyo wanaendelea na mkakati wa kuishusha zaidi.
Mabaraza ya wafanyakazi
Rais Kikwete alisema ni muhimu kuwepo
kwa mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi na kwamba hilo si jambo la
hiyari bali ni lazima kwa mujibu wa sheria za kazi.
"Pamoja na matakwa ya ajira na sheria
za kazi, ni vema idara, wizara na taasisi zikaanzisha mabaraza yao.
"Wale ambao hawajaanzisha mabaraza hayo waorodheshwe na watajwe kwani
kufanya hivyo kutasaidia kuwabaini wale ambao wataonekana hawana mabaraza hayo,"alisema.
Pia alisema wafanyakazi ambao
wanaonekana kupigania mabaraza ya wafanyakazi wamekuwa wakionekana kama
wanajiweka mstari wa mbele kudai maslahi yao hivyo wanatafutiwa namna ya
kufukuzwa au kuhamishwa eneo la kazi.
"Hakuna sekta , kampuni wala idara
ambayo iko juu ya sheria. Kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi ni haki
ya msingi na mbali ya kuwa na sheria lakini Tanzania imesaini
makubaliano ya kimataifa kuhusu mabaraza hayo,"alisema.
Uhusiano kazini
Rais Kikwete alisema kuwa uhusiano
mzuri kati ya wafanyakazi na waajiri hupunguza migogoro maeneo ya kazi
na kwamba matawi ya kazi ni muhumu na lazima yawepo.
Alisema waajiri ambao wanakidi kuwepo kwa matawi hayo sehemu za kazi wachukuliwe hatua.
Rais Kikwete pia alisema wakaguzi ambao wanaonekana kukandamiza wafanyakazi ni vema wakaondolewa.
"Ni jambo baya kuona mkaguzi anaegemea kwa muajiri na kuamndamiza mfanyakazi.Hilo halitakubalika kwani ni kuipaka Serikali
matope,"alisema.
Mawakala
Rais alisema kuwa tabia ya wakala
binafsi wa ajira ambao kazi yao ni kutafutia watu kazi na kuwabana
katika malipo ya mishahara ni dhuluma kwa wafanyakazi.
Alisema wakala binafsi wa ajira kazi
yao ni kuwaunganisha watufata kazi na waajiri na si wao kufanya kazi ya
kuajiri na kisha wao wanapunguza mishahara ya wafanyakazi.
"Huku ni kudhulumu wafanyakazi maana wanakuwa hawana uhuasino na waajiri wao kwasababu tu kuna watu ambao wanajiita
mawakala wanaingia mikataba na waajiri, jambo ambalo ni kinyume na sheria ya wakala binafsi,"alisema.
Pamoja na hayo ,Rais Kikwete alisema
ataimarisha utawala bora kwa kujengwa daraja kati ya waajiri na
wafanyakazi wao huku akitumia
nafasi hiyo kuweka wazi kuwa bodi kwenye mashirika ni muhimu kwani ndio
hufanya uamuzi wa shirika.
"Natambua yapo mashirika ambayo yametambua ushiriki wa wafanyakazi katika bodi lakini kuna mashirika mengine bodi
zake hazina wawakilishi wa wafanyakazi,"alisema.
Madai ya watumishi
Rais Kikwete alisema risala ya
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(Tucta) limezungumzia suala
la madai yao kwa Serikali.
"Tunatambua kuwa kuna madai ya
watumishi wa Serikali.Hili tunaendelea nalo kulifanyia kazi na tumefika
mahali pazuri,"alisema Rais Kikwete.
Madai ya walimu
Rais Kikwete alisema kwa mara ya kwanza wamemuita shemeji. Alikiri ni kweli mkewe Mama Salma ni mwalimu na baada ya
kustaafu, ni ruksa kurudi kazini aendelee kushika chaki.
Hata hivyo, alisema kuwa ili kulipa
madeni ya walimu kazi iliyokuwa inafanyika ni kuhakiki madai yao hayo na
kilichobainika kuna ujanja umekuwa ukifanywa na baadhi ya walimu na
kushirikiana na watumishikwenye maeneo husika.
"Kuna baadhi ya walimu walilipwa madai yao lakini wamerudi kudai tena. Ujanja huu umefanyika na kusababisha kila Serikali
inapolipa madeni yanabaki palepale,"alifafanua Rais Kikwete.
Mshara umechelewa
Hata hivyo Rais Kikwete alisema kuwa walimu wakati wanamuita shemeji walisikika wakidai mishara imechelewa.
Alisema baada ya kusikia hivyo aliuamua kufuatilia na kubaini kumbe mshahara wa mwezi huu kwa watumishi wa
Serikali bado
haijalipwa.
Alifafanua hali hiyo ilimfanya amuulize Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT), Profesa Benno Ndullu lakini alijibiwa kuwa
wao BoT ilishamaliza kazi yake tangu April 24 mwaka huu.
"Asubuhi wakati walimu wanasema mwezi huu mshahara umechelewa niliamua kufuatilia lakini gavana alisema kuwa
wamemaliza kazi yao Aprili 24 mwaka huu.
"Hivyo kuna eneo ambalo limechelewesha lakini tunafuatilia ili mshahara uweze kulipwa kwa watumishi wa Serikali,"alisema.
Wafanyakazi wavivu
Kuhusu wafanyakazi, Rais Kikwete
alisema kuwa kuna malalamiko ya kwamba watumishi wengi wa Serikali ni
wavivu. Sifa hiyo si nzuri na ndio inayotumika kushawishi waajiri
kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya Tanzania.
Alisema suala la kudai wafanyakazi wa
Tanzania ni wavivu ni madai ambayo yanaaminika ,hivyo yanatakiwa
kufanyiwa kazi kwa uzito wake.
"Jambo hili lazima lifanyiwe kazi haraka, viongozi wa maeneo yote lazima wakae na kujadili hili kwa kina.Siamini kama kweli
wafanyakazi wetu ni wavivu kiasi
hicho. Mbona natoa tunzo kwa waliofanya vizuri, lazima mlitazame hili
kwa umakini," alisema Rais Kikwete.
Mchakato Katiba mpya
Rais Kikwete alisema alitoa ahadi ya wafanyakazi kushirikishwa kwenye mchakato wa Katiba mpya, ahadi ambayo ameitekeleza.
Alisema kutokana na idadi kubwa ya
wafanyakazi aliona haja ya kutaka sauti za wafanyakazi zisikike kwenye
mchakato huo kwani ni fursa ya kuzungumzia masuala ya wafanyakazi kwenye
katiba.
"Kazi yangu ya kuteua wawakilishi
wenu niliimaliza ,hivyo kazi kwenu, mimi sipo kwenye Bunge la Katiba.
Kubwa kwenu ninyi watumeni kazi wawakilishi wenu.
"Waambieni wawakilishi wenu waseme ya kwenu mnayohitaji mkiwaacha wanasema ya wengine. Mnayotaka wawakilishi wenu
wayaseme na muone wakisema waambieni,"alisema.
Rais Kikwete alisema wasipokuwa makini wawakilishi wao watatekwa na makundi mengine na wao watakosa wa kuwasemea
na hatimaye wakajutia fursa ya kuwa na wawakilishi 12.
Hata hivyo, alisema anasikitishwa na
mwenendo wa Bunge la Katiba na unaposikia mtu mzima anatukana kutoka
kwenye kichwa chake ujue ana
tatizo.
"Tofauti ya mawazo hainisumbui hata kidogo. Pale lazima mambo yatakuwa tofauti maana kila mtu ana mawazo yake na kundi lake.
"Kwenye mitazamo tofauti ndiko kuna patikana jambo nzuri. Watu walumbane kwa hoja lakini itafika mahali pa kufanya
uamuzi," alisema Rais Kikwete.
Pia Rais Kikwete alisema kuwa
ameongeza siku 60 ili kuhakikisha mchakato huo unakamilika na kama
watashindwa basi utasubiri wengine waje lakini Katiba mpya inahitajika
kupatikana.
No comments:
Post a Comment