Sunday, May 4, 2014

Rais Dk Shein azungumza na uongozi wa Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora katika mkutano wa utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuifahamu vyema dhana ya utawala bora ili wawe mfano wa kuigwa katika kuitekeleza dhana hiyo kwa vitendo. Akizungumza katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi hiyo kwa kipindi cha Julai 2013 na Machi 2014 jana, Dk. Shein alieleza kuwa utawala bora ni dhana pana na ni suala mtambuka hivyo watumishi wa Ofisi hiyo hawana budi kuielewa na kuitekeleza ipasavyo katika utendaji wa shughuli zao za kila siku. Alisisitiza kuwa suala la utawala bora linagusa kila eneo la utendaji na utoaji huduma katika serikali hivyo watumishi wote serikalini hawana budi kuzingatia misingi ya utawala bora katika utendaji wao. Aliongeza kuwa utawala bora ni suala muhimu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na ndio maana uongozi wa Awamu ya Saba ulipoingia madarakani umekuwa ukiimarisha jitihada zilizoanzishwa na uongpzi wa Awamu ya Sita kwa kuunda na kuimarisha taasisi zinazosimamia masuala ya utawala bora nchini. Kuhusu bajeti ya mwaka 2014/2015 ya Ofisi ya Rais na Mawenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Shein amewataka viongozi na watendaji wa Ofisi hiyo kutumia uzoefu wa Mpangokazi wao ili waweze kuandaa bajeti halisi kwa kupanga malengo yanayopomika kwa kuzingatia vipaumbele na matumizi bora ya rasilimali zilizopo. Alibainisha kuwa ni vyema kupanga vipaumbele vichache ambavyo bajeti itaweza kuvigharamia ili hatimae kupata matokeo mazuri na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo Ofisi hiyo itakuwa imekwenda sambamba na mfumo wa bajeti unaozingatia matokeo ambao serikali inaufuata. Katika maelezo yake ya awali Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Dk. Mwinyihaji Makame alikiambia kikao hicho kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita Ofisi imeweza kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa kwa kuweza kutekeleza malengo yaliyopangwa. Alieleza kuwa utekelezaji wa malengo hayo yalizingatia mipango ya mikuu ya maendeleo ya nchi ukiwemo Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini-MKUZA II, Dira ya Maendeleo 2020, Malengo ya Milenia pamoja na Ilani ya Uchaguzi wa CCM mwaka 2010/2015. Alibainisha kuwa pamoja na mafanikio hayo, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi inaendelea kutekeleza jumla ya programu na miradi 14 ikiwemo Mradi wa kuimarisha Mawasiliano Ikulu, Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini Yenye Kuleta Matokeo ya MKUZA II na Kujenga Uwezo wa Utekelezaji wa Taasisi za Serikali. Miradi mingine ni pamoja na Mradi wa Utafiti wa Hali ya Utumishi Nchini, Mradi wa Uimarishaji Sekta ya Takwimu, Mradi wa Kuimarisha Juhudi za Kuzuia Rushwa Zanzibar na Mradi wa Kuoanisha Masuala ya Idadi ya Watu, Afya ya Uzazi, Jinsia na Umasikini. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alirejea wito wake wa kuzitaka Wizara na Idara za Serikali kuongeza umakini katika kupanga malengo ambayo hatimae yanaweza kupimika. Alisisitiza kuwa ni lazima kuwe na uwiano kati ya malengo na shughuli za kufikia malengo hayo ili kupata matokeo yaliyopangwa vinginevyo kasoro katika upangaji malengo zinasababisha Wizara na Idara za Serikali kushindwa kufikia matokeo hayo yanayotarajiwa. Katika kikao hicho alizikumbusha Wizara na Idara za Serikali kuwa malengo ya Wizara na Idara makao makuu hayawezi kuwa tofauti na malengo ya Ofisi kuu za Pemba hivyo katika upangaji wa malengo pamoja na bajeti suala hilo halina budi kuzingatiwa. Alifafanua kuwa Ofisi za Pemba ni sehemu ya Makao Makuu ya wizara na Idara hivyo malengo yao hayawezi kutofautiana ingawa kwa kiasi fulani shughuli zinaweza kutofautiana katika kuyafikia malengo hayo kutokana na mazingira yaliyopo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora katika mkutano wa utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka  Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuifahamu vyema dhana ya utawala bora ili wawe mfano wa kuigwa katika kuitekeleza dhana hiyo kwa vitendo.
Akizungumza katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi hiyo kwa kipindi cha Julai 2013 na Machi 2014 jana, Dk. Shein alieleza kuwa utawala bora ni dhana pana na ni suala mtambuka hivyo watumishi wa Ofisi hiyo hawana budi kuielewa na kuitekeleza ipasavyo katika utendaji wa shughuli zao za kila siku.
Alisisitiza kuwa suala la utawala bora linagusa kila eneo la utendaji na utoaji huduma katika serikali hivyo watumishi wote serikalini hawana budi kuzingatia misingi ya utawala bora katika utendaji wao.
Aliongeza kuwa utawala bora ni suala muhimu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na ndio maana uongozi wa Awamu ya Saba ulipoingia madarakani umekuwa ukiimarisha jitihada zilizoanzishwa na uongpzi wa Awamu ya Sita kwa kuunda na kuimarisha taasisi zinazosimamia masuala ya utawala bora nchini.
Kuhusu bajeti ya mwaka 2014/2015 ya Ofisi ya Rais na Mawenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Shein amewataka viongozi na watendaji wa Ofisi hiyo kutumia uzoefu wa Mpangokazi wao ili waweze kuandaa bajeti halisi kwa kupanga malengo yanayopomika kwa kuzingatia vipaumbele na matumizi bora ya rasilimali zilizopo.
Alibainisha kuwa ni vyema kupanga vipaumbele vichache ambavyo bajeti itaweza kuvigharamia ili hatimae kupata matokeo mazuri na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo Ofisi hiyo itakuwa imekwenda sambamba na mfumo wa bajeti unaozingatia matokeo ambao serikali inaufuata.   
Katika maelezo yake ya awali Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Dk. Mwinyihaji Makame alikiambia kikao hicho kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita Ofisi imeweza kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa kwa kuweza kutekeleza malengo yaliyopangwa.
Alieleza kuwa utekelezaji wa malengo hayo yalizingatia mipango ya mikuu ya maendeleo ya nchi ukiwemo Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini-MKUZA II, Dira ya Maendeleo 2020, Malengo ya Milenia pamoja na Ilani ya Uchaguzi wa CCM mwaka 2010/2015.
Alibainisha kuwa pamoja na mafanikio hayo, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi inaendelea kutekeleza jumla ya programu na miradi 14 ikiwemo Mradi wa kuimarisha Mawasiliano Ikulu, Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini Yenye Kuleta Matokeo ya MKUZA II na  Kujenga Uwezo wa Utekelezaji wa Taasisi za Serikali.
Miradi mingine ni pamoja na Mradi wa Utafiti wa Hali ya Utumishi Nchini, Mradi wa Uimarishaji Sekta ya Takwimu, Mradi wa Kuimarisha Juhudi za Kuzuia Rushwa Zanzibar na Mradi wa Kuoanisha Masuala ya Idadi ya Watu, Afya ya Uzazi, Jinsia na Umasikini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alirejea wito wake wa kuzitaka Wizara na Idara za Serikali kuongeza umakini katika kupanga malengo ambayo hatimae yanaweza kupimika.
Alisisitiza kuwa ni lazima kuwe na uwiano kati ya malengo na shughuli za kufikia malengo hayo ili kupata matokeo yaliyopangwa vinginevyo kasoro katika upangaji malengo zinasababisha Wizara na Idara za Serikali kushindwa kufikia matokeo hayo yanayotarajiwa.
Katika kikao hicho alizikumbusha Wizara na Idara za Serikali kuwa malengo ya Wizara na Idara makao makuu hayawezi kuwa tofauti na malengo ya Ofisi kuu za Pemba hivyo katika upangaji wa malengo pamoja na bajeti suala hilo halina budi kuzingatiwa.
Alifafanua kuwa Ofisi za Pemba ni sehemu ya Makao Makuu ya wizara na Idara hivyo malengo yao hayawezi kutofautiana ingawa kwa kiasi fulani shughuli zinaweza kutofautiana katika kuyafikia malengo hayo kutokana na mazingira yaliyopo.

No comments:

Post a Comment