Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquiline Maleko, akizungumza na waandishi wa haabari kuhusiana na kuingia Ubia na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Kama mdhamini Mkuu wa Mawasiliano wakati wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yatakayo anza 28 Juni na kumalizika Julai 8 mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquiline Maleko na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, wakioneshwa na Mwanasheria wa TanTrade, Godwin Mutahangarwa,(Kushoto) Mkataba wa Udhamini wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yatakayo anza 28 Juni na kumalizika Julai 8 mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquiline Maleko, akipitia Mkataba
wa Udhamini wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam
yatakayoanza 28 Juni na kumalizika Julai
8 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania, Kelvin Twissa (kulia) na katikati ni Mwanasheria wa TanTrade, Godwin Mutahangarwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquiline Maleko, na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, wakibadilishana mkataba wa Udhamini wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yatakayoanza 28 Juni na kumalizika Julai 8 mwaka huu. Kushoto ni Mwanasheria wa TanTrade, Godwin Mutahangarwa.
ZIKIWA zimebakia siku chache kuanza Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (maarufu kama Saba Saba), tayari Mataifa 31 na makampuni zaidi ya 500 yamethibitisha kushiriki katika maonesho hayo.
Mkurugenzi
Mkuu wa TanTrade, Jacqueline Mneney Maleko ametanabaisha hayo katika
hafla ya kusaini Mkataba
wa Udhamini wa Mawasiliano na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom ambao
utawezesha kufanikisha maandalizi na Mawasiliano katika kipindi chote
cha Maonesho hayo.
“Maonesho
haya yamekuwa kiungo kikubwa sana, kwa Makampuni ya nje na makampuni ya
ndani na pia yanatoa
nafasi kwa kampuni hizo kukutana na wateja wao na kuzungumza ana kwa
ana,” alisema na kuongeza. “ Mwaka huu Mataifa 31 na makampuni zaidi ya
500 yamethibitisha kushiriki katika maonesho ya mwaka huu.”
Mkurugenzi
huyo alitoa wito kwa washiriki ambao hawajajiandikisha kwa ajili ya
zoezi la kutafuta washindi
katika makundi mbalimbali kuchukua fomu na kujiandikisha. Zoezi hilo
limepangwa kufanyika kuanzia saa 6.00 mchana tarehe 28 Juni na
kumalizika tarehe 29, Juni 2014.
Bi. Maleko, alihitimisha kwa kutoa wito kwa washiriki kujiandaa kutembelea maonesho hayo ili kupata fursa
za masoko, uwekezaji na ajira. Milango itafunguliwa kuanzia Jumamosi tarehe 28 Juni, 2014.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema,
ushirikiano kati yao na TanTarde umekuwa na manufaa kwani umewezesha
kujenga daraja na kutoa fursa kwa kampuni za ndani na kampuni za nje.
“Maonesho
ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (maarufu kama Sabasaba) ni
fursa ambayo
makampuni huitumia kujitangaza na kukutana na wateja wao ana kwa ana,
Kwetu sisi huu ni uwanja wa kuwadhihirishia wateja na watanzania kwa
ujumla ubunifu tulio nao katika huduma na bidhaa wanazozihitaji.”
Alisema Twissa
“Miongoni
mwa huduma hizi ni M Pawa, ambayo kupitia huduma hiyo tumewawezesha
watanzania
kuwa na akaunti ya benki katika simu zao ambapo sasa wanaweza kuweka
akiba ili kufikia malengo yao na hata kukopa pale wanapohitaji.”
Aidha,
Twissa aliendelea kwa kufafanua umuhimu wa huduma za kifedha kwa njia
ya simu za
mkononi kuwa ni mapinduzi ya mtandao wake unaojivunia mawakala zaidi ya
75,000 wa kuaminika nchi nzima. Mteja kuwa na huduma ya M Pesa ni zaidi
ya benki kiganjani mwake kwani ana uwezo mkubwa wa kufanya miamala ya
fedha ikiwemo kutuma, kupokea na kutoa pamoja
na biashara zaidi ya 600 zilizounganishwa na huduma hiyo.
“Natoa
wito kwa Watanzania kutembelea banda letu kupatiwa huduma na bidhaa
zetu, pia kupata
maelezo juu ya ofa lukuki tulizonazo. Napenda kuwashukuru TanTrade kwa
kuendelea kushirikiana nasi katika kipindi hiki muhimu kwa
wafanyabiashara nchini.” Alihitimisha Twissa.
Maonesho
ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam “SabaSaba” ni maonesho ya
biashara yanayoongoza
siyo nchini Tanzania tu bali katika eneo lote la Afrika Mashariki kwani
huwapatia fursa wafanyabiashara fursa ya kuonyesha na kutafuta masoko
ya bidhaa na huduma walizonazo. Mbali na hapo pia huwakutanisha
wafanyabiashara mbalimbali kujionea bidhaa wanazozalisha
ili kusaidia ubora na ushindani. Maonesho haya yanayofanyika kwa siku
kumi huwavutia wageni zaidi ya 350,000 na kujenga mahusiano mazuri baina
ya watoa huduma na wateja wao. Katika maonesho haya, waoneshaji hupata
fursa ya kukutana na wateja wao na watembeleaji
hupata nafasi ya kuangalia na kulinganisha ubora wa bidhaa, bei,
teknologia na hata kujifunza kutoka kwa waoneshaji mbinu za kuboresha au
kuanzisha biashara zao.
‘ ILI
KULETA MAFANIKIO NA KUHAKIKISHA USALAMA UNAKUWAPO KIPINDI CHOTE CHA
MAONESHO, SILAHA ZA AINA YOYOTE AU MIFANO YAKE HAZITARUHUSIWA
KATIKA UWANJA WA MAONESHO’.
No comments:
Post a Comment