baada ya jeshi la polisi kupata taarifa toka kwa msiri, kuwa kuna gari namba T 178 BSY aina NOAH inasemekana ina mizigo ya wizi. Baada ya taarifa hizo askari walijipanga na kuweka mtego, na kufanikiwa kulikamata hilo , na walipolipekuwa walikuta viroba viwili ,vilivyokuwa na vipande hivyo vya meno ya tembo ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja. Watuhumiwa pamoja na gari husika wanashikiliwa na Watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo:
· ADAM YONA, miaka 37, mkazi wa Mbagala,
· SELEMANI LEONALD, Miaka 37, Mkazi wa M’nyamala,
· HUSSEIN SAID, Miaka 34,
Katika tukio la pili, mnamo 05/06/2014 Polisi Wilaya ya Buguruni mkoa wa kipolisi Ilala kwa kushirikiana na bwana BAKARI YUSUF, Miaka 33, Mhifadhi Wanyamapori Makao Makuu, Mkazi wa Mbezi Beach, walifanikiwa kukamata vipande 28 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya fedha za kitanzania milion mia mbili sabin na tano laki tano na elfu hamsini nyumbani kwa DOMINICK KORINELI maarufu KOMBE, Miaka 35, Mkazi wa Tabata Kisukuru.
Walipofanya upekuzi katika nyumba hiyo ,ambapo kwenye chumba kimoja cha uwani cha bwana HERBERT REVIL MACHAKA, Miaka 30, mkazi wa Morogoro, ndipo kilipitikana kipande 1 cha jino la Tembo.
Upekuzi uliendelea kwenye Stoo na Jiko na walipata vipande 27 vya meno ya tembo na kufanya jumla ya vipande hivyo kuwa 28 kwa tukio la pili hivyo kufanya idadi ya vipande kufikia 54 Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa ujangili huu unaomaliza rasilimali za taifa. na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani
No comments:
Post a Comment