Mnamo Tarehe
01.06.2014 huko maeneo ya Mbagala Maji Matitu,Kata ya Chamazi , Wilaya ya Mbagala, Mkoa wa Temeke, polisi walipokea
taarifa toka kwa mtoa taarifa mwenye namba P.8464 cheo cha Meja FAUDHI OMARI ALLY wa Kikosi cha
Anga Makao Makuu cha JWTZ,
akitaarifu kwamba amemkamata mtu mmoja aitwaye FRANCIS MARTINE
KILALA, Miaka 24, Mkazi wa Kawe akiwa amevaa sare za Jeshi la Wananchi wa
Tanzania zenye cheo cha LUTENI akiwa ndani
ya Daladala.
mtu huyo
alipohojiwa alikiri kuwa yeye sio askari na alipopekuliwa alipatikana na
vitambulisho 3 ambavyo kimoja
chenye no. PT.86876 PTE THOMAS MWITA kikiwa kimewekwa picha yake ya mtuhumiwa , na viwili
vikiwa vya watoto wa askari vyenye namba Z0186 MTUYO OMARI MAGULU na Z0116
MAULIDI ISSA HASSAN ambacho ni cha mtoto wa askari mwenye namba P.8487 NF MANDAGO. Mtuhumiwa
anashikiliwa kwa mahojiano. Upelelezi juu ya wapi amepata sare hizi unaendelea.
Aidha amekamatwa
mtu mwingine aitwaye DAUDI MADA maarufu kama PAKIMERO, Miaka 30, Mkazi wa Tandika Nyambwera akiwa na sare za
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zikiwemo
· FULANA NA SHATI
YA KIJANI
· SURUALI NA SHATI
ZA MABAKA
· JOZI MOJA YA
BUTI ZA JESHI
· KOFIA MBILI ZA
RANGI YA KIJANI
· BEGI MOJA LA
NGUO (MABAKA)
TAARIFA
ZA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM KUANZIA TAREHE 1/6/2014 – 12/6/2014.
·
Idadi ya makosa yaliyokamatwa ilikuwa
7176
·
Pikipiki zilizokamatwa 462
·
Daladala zilizokamatwa 4136
·
Magari mengine 2441
·
Hela za tozo 215,280,000/=
No comments:
Post a Comment