Saturday, July 12, 2014

chuo cha Kilimo na mifugo Kaole chafanya mahafali ya pili leo Julai 12

Na Andrew Chale, Bagamoyo
CHUO  cha Kilimo na Mifugo Kaole (Kaole College of agriculture (KCA), kesho Jumamosi Julai 12, kinatarajia kufanya mahafali yake ya pili chuoni hapo huku wahitimu  291, wakitarajiwa kutunukiwa vyeti mbalimbali.
 
Akizungumza mjini hapa,  principle wa chuo hicho,  Cuthbert Liwa alisema kuwa, tayari maandalizi yamekamilika na mahafali hayo yatafanyika kwenye viwanja vya chuo hiko.
 
“Jumla ya wahitimu 291, wanatarajiwa kuhitimu na kutunukiwa  vyeti vyao.   Kati ya hao, wahitimu 179, fani ya Kilimo na  wahitimu 112, kwa fani ya Ufugaji” alisema Liwa.
 
Aidha, alisema mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, anatarajiwa kuwa Dr. Masuruli wa Wizara ya  Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
 
Aidha, aliwaomba watu mbalimbali kujumuika kwa pamoja kwenye mahafali hayo, chuoni hapo, Kaole, Bagamoyo. (the college is located in South-East Bagamoyo 3.5 km from Bagamoyo township in the premises of Kaole Secondary school.  The centre is along the showers of the Indian Ocean).

No comments:

Post a Comment