picha
ya juu na chini wananchi wa jiji la Arusha waliojitokeza kuuangalia
mwili wa jambazi huyo atari aliowawa na polisi usiku wa kuamkia leo
mwili wa Jambazi hilo ukiwa umelazwa ndani ya gari la polisi mara baada ya kuwawa tayari kwa ajili ya kupelekwa mochwari
wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi hilo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha
baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa jambazi hilo zikiwemo silaha mbalimbali
kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina la Glock Fab Defence moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia
Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan
Abudallah alimaarufu kwa jina la
Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa
Moivo ameuwawa baada ya kupigwa
risasi katika majibizano na askari wa
jeshi la polisi.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha
Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 10 mwaka huu majira ya saa nane na dakika nne
usiku katika kijiji cha
Moivo kilichopo ndani ya
kitongoji cha Enaboishu wilayani
Arumeru.
Alisema kuwa marehemu
Ramadhan Abdallh aliuwa
anatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali
ya uhalifu ambayo yameshawahi kutokea ndani ya
mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hiii.
Alibainisha kuwa
kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na
juhudi na kutumia mbinu za kisasa za kiyupelelezi na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu) ambapo
askari polisi walimwamuru ajisalimishe
lakini alikaidi amri na kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha
askari kujibu mashambulizi na kumsababishia
umauti kumfika.
“Mara
baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza
kumpekuwa mwili wa marehemu na
alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU976
iliotengenezwa
nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14) ambapo alikuwa
ameishika
mkononi pamoja na maganda matano yarisasi
na mbali na hapo polisi pia walifanya upekuzi katika chumba cha
jambazi
hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine
zingine mbili
zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio call moja yeye
nembo ya ITSS/UNICTR pamoja na pikipiki aina ya toyo power king
rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU
pamoja na kofia ngumu”alisema Sabas
Aidha alibainisha kuwa
pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi hilo pia
walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki yenye namba za
usajili T 805 CVD ambapo alibainisha
kuwa jambazi hili lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara pamoja na
chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla
yakupiga risasi (Glock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola pamoja na
koti kubwa jeusi.
Kamanda Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili
lilishayafanya kuwa ni pamoja na tukio lililotekea Augast 6 majira ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya
kwa iddi ambapo mtuhumiwa akiwa na
mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika
kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina
nyumbani kwake ,hu ku tukio lingine
likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo yaoasiti ambapo jambazi huyo akiwa
na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi yam domo na kutokea
kichwani mototo aitwaye Christen NIckson
mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na
baadae majeruhi kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
Kamanda sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake
kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi
na kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.
“arusha sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa
hali na mali kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na
napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga vilivyo
,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia waendelee kuwafichua
wahalifu popote pale ili tuwaangamize
kabisa”alisema Sabas
Mmoja wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya
jambazi hilo Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na blog hi i
alilipongeza jeshi la polisi kwa kuweza
kumuangamiza jambazi hilo kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na
kuwanyima raha kwa jinsi walivyokuwa wanauwa watu.
No comments:
Post a Comment