Katika
Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru maelfu walifurika kwa ajili ya kutambua
jamaa zao ambapo mke na mume ambao ni Elly Kaaya, Ofisa Elimu na
Kumbukumbu wa Halmashauri ya Meru na mumewe Kundaeli Kaaya ambaye ni
mwalimu wa Shule ya Msingi Ndoombo wilayani Arumeru walikuwa ni miongoni
mwa maiti zilizotambulika katika ajali hiyo.
Tukio hiilo
limetokea jana eneo la Madila kwenye Kijiji cha Sing’isi saa 11 jioni
baada ya gari hilo la abiria lililokuwa linatokea Usa River kwenda
Arusha kugongana na lori hilo lililokuwa linatoka Arusha kwenda
Kilimanjaro.
Wengine
waliotambuliwa katika ajali hiyo ni pamoja na Ofisa Elimu wa Taaluma
Halmashauri ya Meru, Zakia Katunga na kondakta wa gari hilo, Simon
Wilenya na abiria Kundaeli Kadoya.
Hadi jana
jioni, miili mingine sita ilikuwa bado haijatambulika, huku mamia ya
watu wakiendelea kufika katika uwanja wa chumba cha kuhifadhi maiti
kutambua miili hiyo.
Hata hivyo,
hadi jana dereva wa gari la abiria alikuwa hajulikana alipo na majeruhi
wengine watatu walikuwa wamelazwa wakiwa mahututi Hospitali ya Wilaya ya
Meru.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa
tukio hilo na kuahidi kesho (leo) angetoa taarifa ya tukio hilo.
Jaji Luhangisa aliteuliwa hivi karibuni, kuwa Jaji na Rais Jakaya Kikwete.
Kabla ya uteuzi huo, alikuwa msajili wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Hiace hiyo kwa upande wa mbele. |
Polisi wa usalama barabarani wakisimamia zoezi la kuiondosha Hiace hiyo kwenda kuhifadhi mahali stahili. |
No comments:
Post a Comment