Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na
mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni mjumbe wa TBN
Mkala Fundikira, Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya
AIMS, Shafiq Mpanja wa AIM, Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na
mjumbe wa TBN Khadija Kalili.
Katika mkutano huo TBN imesema kesho Jumamosi jioni Bloggers
takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika
ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salam kwa ajili ya hafla ya
mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa
Bloggers.
Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo
wakati wa mkutano.
Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili
akizungumza wakati wa mkutano.
Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa
mkutano.
Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya
Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi
za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment