Tunapenda
kuwatangazia wananchi kote nchini hasa katika mikoa ya Dar, Bukoba,
Mbeya, Tabora, Simiyu na Mwanza, ambako viongozi wakuu wa chama watakuwa
na majukumu mbalimbali...
Leo
Jumamosi Land Mark Hotel, Ubungo Wakili Mabere Marando, Prof. Baregu na
Mbunge wa Ubungo Mnyika watahudhuria na kutoa mada kwenye kongamano la
mahafadhali ya vijana wa CHASO wanaotarajia kuhitimu vyuo hivi karibuni.
Kongamano litaanza saa 4.00 asubuhi.
KAGERA;
Katibu
Mkuu Dr. Slaa anaanza ziara ya siku 3 mkoani humo ambapo leo atakuwa na
mkutano wa hadhara mjini Bukoba, kisha Jumapili atakuwa Karagwe na
Jumatatu atakuwa Muleba.
Mbeya Mjini;
Baada
ya ziara iliyomfikisha juzi Rungwe na jana alikuwa Kyela, Mwenyekiti wa
Chama Taifa leo atakuwa Mbeya mjini ambapo atakagua zoezi la
uandikishaji wapiga kira katika vituo mbalimbali ili kujionea hali
halisi inavyokwenda.
TABORA;
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Bara, Prof. Abdallah Safari atakuwa mjini Tabora
siku ya Jumapili ambapo atafanya mkutano wa hadhara baada ya kuhudhuria
mahafali ya CHASO Kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali mjini humo.
Mwanza na Simiyu
Naibu
Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu leo Jumamosi atakuwa mgeni rasmi
katika mahafali ya wanafunzi wa CHASO Chuo Kikuu cha SAUT, kisha
atafanya mkutano wa hadhara mjini Magu na baadae jioni atakuwa na kikao
cha ndani Mwanza Mjini.
Siku
ya Jumapili atafanya mkutano wa hadhara mkoani Simiyu kabla ya kuelekea
wilayani Sengerema Kwa ajili ya kongamano la mafunzo ya vijana wa
CHADEMA kuhusu uzalendo Kwa nchi yao.
TAIFA KUZIZIMA KESHO
Kesho
Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe atatetemesha nchi kwa kuzungumza na
Taifa kupitia mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika viwanja vya
Tanganyika Packers Kawe DSM.Mkutano huo utarushwa moja kwa moja na ITV
Tunaomba wananchi na wafuasi wetu kote nchini waendelee kuunga mkono chama chao
No comments:
Post a Comment