Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mwanamuziki
Diamond Plutnamz pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Clods FM Bw.
Ruge Mutahaba wakati wa matembezi ya mshikamano kwa ajili ya uzinduzi
rasmi wa kampeni ya usafi wa jiji la Dar es salaam itakayofanyika kwa
siku 90 ikishirikisha wenyeviti wa mitaa, wananchi katika maeneo yao,
Taasisi za Serikali na Mashirika Binafsi ili kuhakikisha jiji la Dar es
salaam linakuwa safi kabisa.
Makonda
amewaambia wananchi mara baada ya matembezi hayo kwamba Dar es salaam
bila uchafu inawezekana na amenzisha shindano kwa wenyeviti wa mitaa
iliyopangwa na isiyopangwa mwenyekiti atakayeshinda kwa usafi katika
eneo lake atajishindia shilingi milini 50.000.000 na mwenyekiti
atakayekuwa wa mwisho katika eneo lake atapata nafasi ya kutangazwa
katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na uchafu uliopo katika
eneo lake na wananchi wake na pia mazingira hayo machafu yataonyeshwa
yakiambatana na picha za mwenyekiti huyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya
ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio
Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia
ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya
ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio
Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia
ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Diamond
Plutnamz huku ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati wa matembezi hayo
yaliyofanyika leo kwa ajili ya kuhamasisha wakazi wa jiji la Dar es
salaam kufanya usafi katika maeneo yao.
Haya
ni miongozi mwa matukio yaliyojiri wakati wa matembezi hayo ya
kuhamashiwa wakazi wa jiji kufanya usaifi ambapo kampeni maalum ya siku
90 za kufanya usafi zimezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Paul Makonda.
Wapiga
picha waliendelea na ubunifu wa kutafuta picha nzuri kama
wanavyoonekana hapa kwenye picha wakiwa kwenye pikipiki wakipiga picha
katika matembezi hayo.
Baadhi
ya washiriki wa matembezi hayo wakifanya mazoezi mara baada ya kuwasili
kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambako ndiko kampeni
hiyo ilikozinduliwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akishiriki katika mazoezi
hayo mara baada ya mtembezi hayo kuwasili katika viwanja vya Leaders
Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na viongozi wa
dini waliofika katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambao ni Sheikh Mkuu wa
Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim na Askofu David Mwasota kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi
Kikundicha ngoma kikitumbuia katika uzinduzi huo
No comments:
Post a Comment