Shujaa Wetu,
Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude
Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na
kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.
Alihudhuria
Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi
(Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana
duniani.
Kutoka
Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto
na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa
Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.
"Kitu
ambacho nimejifunza ni kupata kujiamini zaidi kwa sababu ule Mkutano
ulihudhuriwa na watu wengi, wakiwepo viongozi kutoka zaidi ya nchi 170
wanachama wa Umoja wa Mataifa. Wameniasa kusoma zaidi ili kufikia
malengo yangu ambapo nitaendelea kuzungumza na wananchi pamoja na
viongozi wao juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo nitakuwa
balozi wao". Alisema Getrude.
"Wazazi
wawaruhusu watoto wao katika kushiriki shughuli mbalimbali za vikundi
ili waweze kujiamini zaidi katika kufikia ndoto zao". Anasema Mtoto
Mwanahabari Getrude.
Shabani
Njia (Kulia) ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani
Mwanza MYCN akizungumzia mapokezi ya Mwanahabari na Balozi wa Mazingira
wa Umoja wa Mataifa akiwakilisha kundi la Watoto na Vijana Getrude
Clement
Clement Leon ambae ni baba mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza.
Rizik
Athman ambaye ni mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae
katika Uwanja wa ndege Mwanza ambapo anafurahishwa na hamasa aliyonayo
mtoto wake ikiwemo kujiamini katika masuala mbalimbali ikiwemo ya
habari.
Getrude (katikati) akiwa na wazazi wake, Clement Leon (kushoto) pamoja na Rizik Athuman (kulia).
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, mapema wakifurahia jambo wakati wakimsubiria Getrude.
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN wakiwa pamoja na Getrude.
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, wakifurahia na Getrude katika picha ya pamoja.
Mapokezi ya Mtoto Getrude.
Mapokezi ya Mtoto Getrude.
Mapokezi ya Mtoto Getrude, Wengi walimsubiria kwa hamu kubwa.
Shuja, Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa UN Getrude Clement baada ya kuwasili Jijini Mwanza.
Tazama HAPA Getrude akihutubia katika Mkutano wa UN.
No comments:
Post a Comment