Na Chalila Kibuda, Globu Jamii.
IDARA
ya Uhamiaji nchini imekutana na Idara ya Uhamiaji ya nchini Zambia
kujadili masuala ya uhamiaji kati nchi mbili juu wananchi katika nchi
hizo kufuata taratibu za uhamiaji.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Idara ya
Uhamiaji na Msemaji wa Idara hiyo, Abbas Irovya amesema kuwa kuna
watanzania walikamatwa nchini Zambia 4000 ambao walikuwa
wanajishughulisha na ususi.
Irovya
amesema kuwa kuna watu wanaghushi hati ya kusafiria na kudai kuwa
wanataiboresha ili wasiweze kughushi hati hizo na wataobanika kuwa na
hati hizo watachukuliwa hatua katika vyombo dola.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji wa Zambia, Moola Milomo amesema kuwa kuna
fursa za ususi nchini humo na kutaka watanzania kufuata utaratibu wa
idara ya uhamiaji.
Amesema kuna changamoto kwa watu wanaoingia nchini Zambia lakini Tanzania na inakabiliwa nazo hivyo kunahitaji utatuzi.
Naibu Kamishna wa Idara Uhamiaji, Abbas Irovya akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maswala mbalimbali
yanayojitokeza kwenidara hiyo kati ya Tanzania na Zambia.
Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Abbas Irovya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji nchini Zambia, Moola Milomo.
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji nchini Zambia, Moola Milomo akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kumaliza
mkutano wa kujadili masula ya uhamiaji kati ya nchi Zambia na Tanzania.
Kushoto ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya.
Baadhi
ya Watendaji mbalimbali Idara ya Uhamiaji wa Tanzania na Zambia wakiwa
katika mkutano wa kujadili masuala ya uhamiaji kati ya nchi ya Tanzania
na Zambia katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment