Bunge nchini Iraq limemchagua
spika mpya kama hatua ya kwanza ya kumaliza mzozo wa kisiasa ambao
umelinyima taifa hilo serikali yenye ufanisi wakati huu ambapo
inakabiliana na wanamgambo wa kisunni.
Spika huyo mpya ni salim Jabouri ambaye alikuwa mgombea wa dhehebu la kisunni.Bunge pia linatarajiwa kumchagua rais mpya wa dhehebu la Kikurdi pamoja na waziri mkuu wa Kishia ambao ni wadhfa ulioligawanya taifa hilo huku waziri mkuu wa sasa Nouri Al malik akisisitiza kuwa hatojiuzulu licha ya shinikizo za kitaifa na kimataifa afanye hivyo.
Awali waziri wa masuala ya kigeni katika eneo linalojisimamia la Kikurdi nchini humo Falah Mustafa Bakir ameitaja nchi hiyo kama iliyofeli na kumlaumu waziri mkuu Nouri Al malik.
Bwana Bakir amesema kuwa Iraq itagawanywa katika maeneo matatu huku kukiwa na eneo huru la kikurdi.
No comments:
Post a Comment