Tuesday, July 15, 2014

Israel yaanza kushambilia Gaza tena



Israel imeanza tena kushambulia Gaza ikidai kuwa Hamas inaishambulia licha ya mkataba wa kusitisha vita kufikiwa.
Awali Israel ilikubali kusitisha vita kufuatia pendekezo la Misri kwa pande zote mbili kusitisha vita Jumanne asubuhi.
Hata hivyo, kundi la Hamas, ambalo linadhibiti Gaza, lilikataa makubaliano hayo na kusema ni kama kusalimu amri.
Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu 192 wameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel siku nane zilizopita ili kukomesha wapiganaji wa Hamas kuusha makombora nchini Israel.
Raia wanne wa Israel wamejeruhiwa vibaya tangu mashambulizi hayo kuanza , lakini hakuna taarfa zozote za vifo.
Wizara ya usalama nchini Israel imesema kuwa roketi 50 zimerushwa ndani ya Israel tangu isitishe vita.
Mashambulizi ya hivi punde yamepiga maeneo mawili katika ukanda wa Gaza.
Kundi la Hamas lilisema kuwa hawajapokea pendekezo lolote la kusitisha mashambulizi.
Aliongeza kwamba Hamas inahitaji masharti yake yote kukubaliwa kabla ya kukubali kusitisha vita.
Idara ya usalama nchini Israel imekubali mapendekezo hayo lakini ikasisitiza kuwa itaendelea kushambulia Gaza ikiwa Hamas watasitisha kusidhambulia kwa roketi.

No comments:

Post a Comment