Wednesday, February 26, 2014

Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal atembelea mradi wa majiko sanifu na kuzuru kaburi la Sokoine

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange juu ya kusafisha na kuyafanya maji kuwa salama, wakati alipotembelea sehemu ya karakana hiyo inayotumia umeme wa nguvu za jua (Solor Power Energe).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Bw. Kisioki Moitiko kuhusu utengenezaji wa majiko hayo, wakati alipotembelea kwenye karakana hiyo leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya kwanza Marehemu Edward Moringe Sokoin wakati alipozuru kijijini kwa marehemu Monduli juu alipokua katika ziara ya kikazi Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya kwanza Marehemu Edward Moringe Sokoin wakati alipozuru kijijini kwa marehemu Monduli juu alipokua katika ziara ya kikazi Wilayani Monduli Mkoani Arusha 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya moja ya nyumba zinazotumia majiko sanifu wakati alipotembelea katika kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha leo.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akicheza ngoma ya kimasai na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dkt. Binilith S. Mahenge, akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani Arusha, ambapo ameambatana na Makamu wa Rais kwenye ziara hiyo.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kifimbo kutoka kwa wazee wa kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha leo February 25-2014, mara baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kabila la kijiji hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha baada ya kuwahutubia  mkutano wa hadhara leo February 25-2014.

No comments:

Post a Comment