PICHA JUU NI MTUNZI NA MSHAIRI PROFESSA EBRHIM HUSEIN
Kamati ya
usimamizi wa Tunzo ya Ushairi ya Ebrahim
Hussein ,kwa kushirikia
na na Tanzania Gatsby
Trust (TGT) na Mkuki na Nyota Publishers ,inapenda kutangaza kwa umma
uzinduzi wa shindano jipya la ushairi
Lengo kuu la
shindano hili ni kumkumbuka mwanzilishi wa Tunzo hii ,Marehemu Geralnada Belkin,mpiga filamu
wa Canada aliyeishi Tanzania katika
miaka ya 1970 .Bwana Belkini aliipenda lugha na fasihi ya Kiswahili naalifanya
kazi na mtunzi Ebrahim Hussein kuikuza.Alichangia mfuko akitaka uwe chachu ya kuendeleza
Kiswahili,hasa utunzi wa mashairi.TGT ,shirika linalosimamia mfuko huu ,imewashirikisha wajumbe
wa kamati kutoka Mkuki na Nyota Publishers pamoja na wanazuoni mbali
mbali wa ushairi katika kuendesha shindano hili lililofunguliwa rasmi leo
tarehe 26/02/2014
MALENGO
MAKUBWA YA SHINDANO HILI.
·
Kuuenzi
mchango wa mtunzi,mwanafasihi ,mwanatamthilia ,mtengeneza filamu na
mwalimu mashauri TANZNAIA proffesa
Ebrahim Hussein
·
Kukuza
fasihi na lugha ya Kiswahili kwa
kuibua na vipaji
vya watunzi wa mashairi na nyimbo
·
·
Kuongeza
idadi ya maandikabla ya mwezi augustshi ya bora katika hazina ya vitabu vya
Kiswahilili .
la majaji limeundwa kwa ajili ya kupitia tungo
na kuhagua washindi.Majaji wataalam wa lugh ya Kiswahili na ushairi,wakiwamo waalimu wa
fasihi,wataongozwa na misingi ya kutokuwa na upendeleo.vijana na washair wa
tungo za iana mbali mbali (ya kijadi,ya kisiasa )wanakaribishwa kushiriki kila
mmoja bila kujali umri ,jinsia ,kazi dini na ulemavu au mnahali anapotoka
anakaribishwa kushiriki katika shindano hili.
Shindano
litafunguliwa 30 mei 2014 ,na washindi watatangazwa kabla ya mwezi Agosti
,Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi 2000,000?= mshindi wa pili Atapata 1300000/= na watatu 70000/=
Melezo ya
tunzo hii
1.hili ni
shindano la ushairi katikaq lugha ya KISWAHILI
2.Kwa mwaka
Huuu tungo zitakazo shirikiahwa ni aina mbili
tu:maishairi na Nyimbo
MASHAIRI
Yanaweza
kuwa:
a)Ya
kimapokeo yenye kuzingatia kanuni na
urari wa vina na mizani kama zilivyofafanuliwa na Amri Abedi na wataalam
wengine AU
b)Mashairi
Huru (masivina)yasiyozingatia kanuni za urari wa vina na mizani
2.2 NYIMBO
a) Zinaweza
kuwa kimapokeo zenye kuzingatia kanuni
za bahari ya wimbo katika ushairi wa
kiswahili (k.m. zile za taarabu)
b)Za kizazi
kipya “(mathalani zile za hip hop,bongo fleva )
MUHIMU ;
Tenzi /Tendi hazitahusika katika shindano
hili,Aidha ,kazi za kinathari
,kama riwaya au tamthilia ,hazitahusika.
3.0 VIGEZO
Kila mshiriki awasilishe mswada MMOJA tu wenye tungo TATU
tu,mswada wenye Tungo Zaidi ya tatu hutashughulikiwa wala kushindanishwa.
3.1 Tungo ziwe ni za mtunzi mwenyewe ,zisiigwe au
kunakiliwa kutoka kwa mtunzi au watunzi
wengine.
3.2 Tungo ziwe mpya kabisa .yaani
,zisiwe zimepata kuchapishwa katika magazeti ,magazine,majarida au vitabuni ,kutiwa katika CD au kanda kucheza jukwaani, redion au kutangaIzwa na kusambazwa
kupitia katika mitandao
3.3 Kila
Utungo wa kimapokea uzingatie kanuni za
kijadi za utunzi ,na usipungue beti 10 au kuzidi 15.
3.4 Utungo
wa wimbo ,pamoja kuzingatia kanuni zinazohusika ,usipungue beti 3 wala kuzidi
beti 10
3.5 Utungo huru usipungue
mishororo(mistari )3 wala kuzidi
mishororo 50.
3.6
Mtunzi atachagua mwenyewe
mada na maudhui ya utungo wake.
3.7 Tungo
ziheshimu miiko ya kijamii na kimaadili
4.0 VIGEZO VYA USHINDI
JOPO LA
WAAMUZI LITAZINGATIA VIGEZO VIFUATAVYO:
1)Usaili:Ni kazi ya mtunzi mwenyewe?
2)Lugha na mtindo :Ufasaha na upekee
3)Uzingativu
wa kanuni za bahari /aina ya utungo inayohusika
4)Uzito wa
fikra na maudhui ,na usadifu wake kwa
jamii
5)Mguso na hisia ,na mvuto kwa msomaji
|
No comments:
Post a Comment