Wednesday, February 26, 2014

Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka kundi la walemavu, Fredyrick Msigallah akisukumwa na mwenzake Bure Zahran kuelekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kusikiliza uwasilishwaji wa Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wajumbe Anna Abdalla na Paul Kimiti, wakizungumza jambo wakati wakielekea kwenye ukumbi huo. 
Wajumbe Anne Makinda na Frederick Werema, wakijadili jambo nje ya ukumbi wa Bunge kabla ya kuingia ukumbini kuhudhuria kikao cha Bunge Maalum la Katiba leo. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar, wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuhudhuria kikao hicho cha kuwasilisha Rasimu ya Kanuni za bunge hilo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto), akijadili jambo na wajumbe wenzake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) na Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia, ndani ya ukumbi wa bunge hilo leo. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiipitia Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, mara baada ya kugaiwa na kabla ya kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Costa Mahalu. 

Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, akiendesha kikao kilichokaa kama semina kwa ajili ya kuwasilishwa Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, Mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, akiendesha kikao kilichokaa kama semina kwa ajili ya kuwasilishwa Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, Mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, Profesa Costa Mahalu akiwasilisha risimu hiyo, wakati wa kikao kilichokaa kama semina kwa wajumbe wa Bunge hilo leo. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, Profesa Costa Mahalu akiwasilisha risimu hiyo, wakati wa kikao kilichokaa kama semina kwa wajumbe wa Bunge hilo leo. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Julias Mtatiro, akichangia kuhusu kuaghirishwa kwa bunge hilo, ili kutoa muda wa kuipitia rasimu hiyo, kabla ya kuanza kuijadili jioni.

No comments:

Post a Comment