picha na maktaba aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda ambaye uteuzi wake umefutwa
mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha na anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu jijini Dar es salaam
Na Woinde Shizza, Arusha
Hatimaye mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda uteuzi wake umefutwa na
Rais John Magufuli ambapo mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo
ataapishwa kesho kuwa mkuu mpya wa Mkoa huo imefahamika.
Hata hivyo kuna ishara zote kuwa mvutano uliojitokeza kati ya mkuu
wa zamani Ntebenda na UVCCM mkoani hapa ndiyo ulioachangia kwa
kiasi kikubwa RC huyo kung'olewa.
Uchunguzi wa weti unebaini kuwa sakata la wapangaji kulipa kiasi
kidogo cha fesha katika mradi wa maduka ya UVCCM , mikataba mibovu na
mkuu wa mkoa kumpigia simu katibu wa Uvccm Mkoa wa Arusha Ezekiel
Mollel akimtaka ache kuwabughudhi wapangaji kunatajwa ndiko
kulikoiudhi ikulu na kufukuzwa kazi.
Jambo jingine ambalo pia linatajwa na wadadisi wa mambo yakisiasa
mkoajini hapa ni mfululzo wa matukio ya uchomaji moto katika shule
tano za sekondari huku RC akionekana kutochukua hatua muhimu za
kuyakabili masuala hayo.
Mapema wiki ya juzi katibu wa Uvccm Ezekiel Mollel aliitisha mkutano
na waandishi wa habari na kumtaka aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha
Ntibenda aaache mara moja kumpigia simu za vitisho ili kuwalinda
wapangaji wasiotendea haki uvccm katika malipo ya miradi yake badala
yake ampigie simu za kupambana na hujuma, ufisadi aidha dhidi ya mradi
ya chama au ile ya serikali .
Kwa upande wake mwenyekiti w a UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya
naye alisema kuwa wanamshukuru Rais Wa nchi hii ambaye pia ni
mwenyekiti wa CCM taifa kwa kusikia kilio cha wana arusha na kuamua
kumtoa mkuu huyo wa mkoa na kuleta mungine .
Napenda kuchukuwa nafasi hii kumpongeza rais wa nchi hiii kwa kumuona
mkuu huyu wa mkoa kuwa ni jipu afai kwani kuna mambo mengi ambayo
ameyafanya yasioyofaa tunamuhaidi kumuuunga mkono na kumpa
ushirikiano wa kutosha mkuu mpya wa mkoa Mrisho Gambo " Alisema
Sabaya.
Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumpa ushirikiano wa
kutosha mkuu huyu wa mkoa kwani ni mchapakazi na pia ni mtenda haki .
Naye katibu hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emanueli Kiusa alisema kuwa wao vijana wa chama cha mapinduzi hawatakuli kuwa na kiongozi mzigo ,fisadi na ambaye anapenda rushwa na asiyesimamia haki na iwapo kama kunakiongozi wa namna hiyo ndani ya chama ajitoe mapema maana UVCCM wakimgundua hawata muacha .
Alisema kuwa anaamini mkuu mpya wa mkoa anatambua kazi aliotumwa kuwafanyia wananchi hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Arusha ,viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa serikali kumunga mkono kwa kumpa ushirikiano ili aweze kufikisha mbali mkoa watu na kuwafanyia watu wa Arusha mambo makubwa ya kimaendeleo .
No comments:
Post a Comment