Friday, August 19, 2016

Watoto wenye saratani wapatiwa msaada.


Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo akiongea na wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani (Hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili,(kushoto) ni Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza na (kulia) ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza akiongea na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa kusaidia watoto wanaotibiwa ugonjwa wa Saratani  katika hospitali ya Muhimbili.Wafanyakazi wa Vodacom pia walitoa msaada wa fedha taslimu,vyakula na vitu mbalimbali vya kuwasaidia ambapo pia walitenga muda wao kusafisha maeneo ya hosteliwanazoishi watoto hao na walishiriki kuwatengenezea lishe na kucheza nao kwa ajili ya kuwapatia faraja.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania katika picha ya pamoja  muda mfupi baada ya kushiriki katika kazi za kijamii za kusafisha mazingira  ya hosteli wanazoishi watoto wanaotibiwa Saratani katika hospitali ya Muhimbili ambapo pia waliwatengenezea lishe na kucheza nao,vilevile walijitolea fedha zao kununua mahitaji mbalimbali ya watoto hao.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakishiriki kusafisha  mazingira  ya hosteli wanazoishi watoto wanaotibiwa Saratani katika hospitali ya Muhimbili
 Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza na (kulia) akiongea na wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani (Hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili (katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo na kulia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan
 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan (Kulia) akiongea na wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani (Hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili (katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo na (kushoto ) ni Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza.
 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan (Kulia) akipokea baadhi ya vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi wa Vodacom kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza (wa nne kutoka kulia) wengine pichani wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo (Wa tatu kutoka kushoto).Wengine ni maofisa wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na Saratani.
 .Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakicheza na watoto.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakishiriki kutengeneza lishe wakati walipojitolea muda wao kusaidia watoto wahanga wa ugonjwa wa Saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya saratani ambao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepatiwa msaada wa milioni 20 kutoka taasisi ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya kufanikisha  matibabu yao na kuwapatia lishe bora.

Mbali na msaada wa fedha wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania wametenga muda wao kushiriki kusafisha maeneo ya hosteli wanaoishi watoto hao ikiwemo kucheza nao,kuwatengenezea lishe pia wametoa msaada wa vyakula na fedha taslimu kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto hawa.

Msaada huo  umetolewa leo  katika hosteli wanazoishi watoto hao zilizopo katika  hospitali ya Taifa Muhimbili  kupitia Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwahudumia watoto wenye maradhi ya Saratani linalojulikana kama Tumaini la Maisha ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto  kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo.

Akitoa pongezi kwa niaba ya serikali,Dk.Msemo amesema kuwa serikali inafarijika inapoona makampuni  ya biashara kama Vodacom yanajitoa kusaidia jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali hususani katika sekta ya afya ambako kunahitajika uokoaji wa maisha ya watu.
“Nawapongeza  sana wafanyakazi wa Vodacom na taasisi yake yake ya kusaidia masuala ya kijamii ya Vodacom Tanzania Foundation pia nimefurahishwa kuona wafanyakazi mmejitoa kuchangia kusaidia watoto hawa wenye matatizo ya saratani na kutenga muda wenu kuja kusafisha mazingira eneo hili wanaloishi,kushiriki kuwatengenezea lishe na kujumuika nao kwa kucheza nao kwa ajili a kuwapatia faraja”.Alisema.

Akiongea wakati wa kupokea msaada huo Mkurugenzi wa Shirika la Tumaini la Maisha,Dk. Trish Scanlan alishukuru kwa msaada huo kutoka Vodacom Tanzania Foundation kwa watoto utakaowafikia na kuwanufaisha walengwa kupitia  shirika hilo lisilo la kiserikali linaloshughulika na kuwasaidia watoto wahanga wa ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 Alisema kuna idadi kubwa ya watoto zaidi ya 300 wanaolazwa hospitalini hapo wakiwa wanakabiliwa na saratani ya aina mbalimbali na kutokana na umri wao  na wanahitaji misaada ya  madawa ya kuwatibu ikiwemo lishe bora na mahitaji mengine mengi ya kila siku.

Kwa upande wake Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza alisema kuwa siku zote taasisi hiyo itakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali katika kusaidia jamii hususani katika nyanja za Afya na Elimu.

“Afya ni moja ya suala ambalo tunalipa kipaumbele na ndio maana tumekuwa tukivalia njuga kutokomeza magonjwa mbalimbali mojawapo ikiwa ugonjwa huu wa saratani ambao siku hadi siku umekuwa ukiongezeka na kusababisha vifo vya watu wengi ”Alisema.

Alisema Vodacom Foundation imetoa kiasi cha shilingi milioni 20 kupitia taasisi ya Tumaini la Maisha ili kuwawezesha watoto hawa kupatiwa  madawa,lishe  bora na mahitaji mbalimbali hususani katika kipindi hiki kigumu wanachoendelea kupata matibabu na aliwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia wenye matatizo mbalimbali kwenye jamii.

 Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake anaendelea na matibabu ya Saratani Grace Nyambisu kutoka mkoani Dodoma akiongea kwa niaba ya wenzake alishukuru Vodacom Tanzania Fondation kwa msaada huu muhimu wa lishe na madawa kwa watoto wao katika kipindi hiki kigumu ambacho wanaendelea kupata matibabu.

Alisema kwa msaada huo  taasisi hiyo imethibitisha usemi wa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki kwa kuwa umetolewa katika muda mwafaka ambao watoto wanahitaji kupata lishe bora na madawa wakati huohuo wazazi wengi wakiwa wanakabiliwa na changamoto ya kutomudu kuwahudumia  kutokana na kukabiliwa na ugumu wa maisha ambao unasababishwa na kutumia muda wao mwingi kuuguza watoto badala ya kujishughulisha na kazi za uzalishaji kwa ajili ya kuwaingizia vipato.

No comments:

Post a Comment