Tuesday, October 18, 2016

DALILI ZA USONJI BADO NI TATIZO KWA TANZANIA


 Mkuu wa kitengo watu wenye tatizo la ugonjwa wa Usonji (National Association for People with Autism –Head)  Dkt Stella Rwezaula (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua warsha maalum kwaajili ya kuoa uelewa kwa watu mbalimbali kuhusu tatizo la Usonji nchini, anaefuata ni Dialla Kassam ambaye ni kurugenzi wa kituo cha Afya cha LOTUS ambao ndio wazamini wa warsha hiyo, akifuatiwa na mtaalam wa mambo ya usonji dunia bw, Kevin Baskerville, kutoka Leicestershire, UK, pamoja na Meneja wa kituo cha Lotus Bi Deepack Gorecha kushoto.
Wapili toka kushoto ni Mtaalam wa mambo ya Usonji toka UK bw, Kevin  Baskervile akikabidhi mfumo maalum alioubuni kwaajili ya kusaidia kufundisha watoto wenye usonji kwa dokta Stela Rwezaula toka muhimbili ili kusaidia kufundisha watoto wanaopatwa na tatizo hilo kupata elimu kwa njia ya picha. katikati anaeshuhudia ni mkurugenzi wa kituo cha afya kinachosaidia watoto wenye usonji Bi Dialla Kassam na Deepak Gorecha (kushoto) wakishuhudia. Aliyesimama ni Mtaalam wa tatizo la  Usonji toka UK bw Kevin  Baskervile toka UK akitoa mada kwa wadau mbalimbli wakati wa warsha maalum kwaajili ya kueneza uelewa kuhusiana na tatizo la usonji nchini.
 Wapili toka kulia ni mkuu wa kituo cha afya kinachosaidia wagonjwa wa Usonji nchini Bi Dialla Kassam akiongea na waandishi wa habari kuhusu udhamini wao wa warsha maalum ya kuongeza uelewa wa usonji kwa wadau mbalimbali nchini wakiwemo wazazi, anaefuata ni mtaalam wa tatizo la usonji toka UK bw, Kevin Baskerville, Meneja wa kituo cha afya cha LOTUS bi Deepak Gorecha na Mkuu wa kitengo kinachoshughulikia watoto wenye usonji dkt Stella Rwezaula.
  • Usonji bado changamoto kubwa Tanzania


Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na ugonjwa wa usonji ambao wengi hawautibu kutokana na kutoelewa dalili zake, imefahamika.
Hili lilielezwa na mkuu wa Chama Cha watu wenye Usonji Kitaifa (NAPA-T) Dr Stella Rwezaula katika mkutanona waandishi wa habari. 
 “Dalili za usonji bado hazijafaamika vizuri kwa wazazi na walimu nchini hivi wanashindwa kuutibu ugonjwa huu au kupata msaada wa kitaalamu kwani ni ugonjwa ambao una mambo mengi yanayoathiri namana mtu anavyowasiliana na mara nyingi huwa na tabia ya kufanya vitu kwa kurudia rudia bila kukusudia,” alisema.
 Alisema kwa mwaka huu, kituo cha Afya cha Lotus (LHC), ambacho sio cha serikali na kinafanya kazi za kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu, kimeifadhili NAPA-T kufanya warsha inayolenga kutoa elimu kuhusu usonji na warsha hii itawaleta pamoja washiriki takriban 100 kutoka sekta binafsi na za kiserikali. “Hu ni moja wa mkakati wa LHC kutoa elimu katika jamii na kuwaleta pamoja watoto na wazazi wenye mahitaji maalumu,” alisema.
 Alisema mojawapo wa kazi za NAPA-T kwa kushirikiana na LHC ni kutoa elimu na mafunzo ya kutosha kuhusu ugonjwa huu ikiwemo katika serikali na mitaa na serikali kuu. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa LHC, Dialla Kassam, alisema wanajivunia kufanya kazi na NAPA-T na kumshukuru mfadhili kutoka Uingereza, Kevin Baskerville, ambaye ni mtaalamu wa ugonjwa huu wa usonji, kwa msaada wake kwani amekuwa akija Tanzania mara kwa mara kutoa mafunzo na elimu kuhusu usonji.
 “Kupitia warsha iliyoandaliwa na LHC mwaka jana, International School of Tanzanyika (IST) ilishirikiana na  Shule ya Msimbazi Mseto ya watoto wenye mahitaji maalumu  na watoto wa Msinbazi Mseto sasa wanaruhusiwa kwenda IST kuogelea matra moja kwa wiki,” alisema na kuongeza kuwa LHC inafaya kila jitihada kuunganisha shule zenye mahitaji maalumu na shule za serikali. 
 Alisema LHC pia imekuwa ikitoa msaada kwa shule ya watu wenye Usonji ya Mbuyuni kwa kupitia wataalamu wa kujitolea kutoka pembe zote za dunia na kusimamiwa na LHC ambayo pia hutoa rasilimali za elimu kwa shule hiyo.     
“Kwa msaada wa Kevin, tumeweza kujenga ushirikaino wa muda mrefu na shule ya watoto wenye mahitaji maalumu iliyoko uingereza iitwayo Hope School iliyoko Newark ambayo imeahidi kuendelea kutoa msaada wa vifaa  na mafunzo kwa shule ya Msimbazi Mseto ambayo ni ya serikali,” alisema.
 Alisema LHC pia inafanya kazi kwa karibu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hasa kitengo cha watu wenye matatizo ya akili, ili kutafuta wafadhili ili kuanzisha kituo cha kwaza kabisa cha watu wenye mahitaji maalumu nchini. Kituo hicho kitakuwa na wataalamu wa kutosha ambao watakabiliana na matatizo mbalimbali ya kiakili ikiwemo usonji.
Baadhi ya dalili za usonji ni mtoto kutoweza kumtizama mtu machoni, kutoitika wakati  anaitwa, kushindwa kucheza na watoto wenzake wenye umri sawa, kushindwa kuwasiliana na wenzake, kukataa kubebwa na kukumbatiwa, kutamani kuwa peke yae muda wote na kushindwa kuonesha au kuelewa hisia mbalimbali.

Dalili nyingine ni tabia kubadilikabadilika, kuwa mgomvi, kutopenda mabadiliko, kuchelewa kuzungumza, kurudiarudia mambo Fulani kama vile kutikisa kichwa, kuchezesha mikono, kunyatanyata na kuzungukazunguka.  

No comments:

Post a Comment