KILA Baada ya Mwezi kikundi cha Tandale Youth Development Centre hufanya Jukwaa la Vijana ambapo vijana hukutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na wao. Katika jukwaa la mwezi huu kulikuwa na mada inayosema: "Nafasi ya mtoto wa kike katika jamii" ambapo majadiliano yalilenga zaidi kutambua nafasi hizo, changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike pamoja, namna ya kuzitatua na jinsi gani mtoto wa kike anavyoweza kusimamia malengo yake kufanikiwa.
Aidha katika jukwaa hilo la vijana Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation kupitia Mkurugenzi Mkazi wa hapa nchini, Martha Nghambi alitoa pia elimu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha amani ndani ya familia, ambapo alisema kuwa ili amani iweze kudumishwa na watu waishi bila kuwepo na mifarakano ni lazima kujenga mahusiano mazuri kuanzia chini yaani wanafamilia kuweza kuelewena kwa kuwahusisha wazazi na watoto ambapo hawa wakiishi vema basi hakutakuwa tena na uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa kila mtu analojukumu la kulinda amani.
Mwendeshaji wa Jukwaa la Vijana lililofanyika Tandale leo Jamal Magabilo akitoa neno la utangulizi na kuwakaribisha wageni waalikwa wote katika jukwaa.
Mkurugenzi wa Gida Rahma Bendera akiitambulisha rasmi mada katika Jukwaa la vijana inayosema nafasi ya mtoto wa kike katika jamii.
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi akitoa Elimu kwa kina juu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha amani kwenye familia ambapo aligusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na visababishi vya uvunjishi wa amani pamoja na namna ya kuzuia uvunjifu huo wa amani katika familia.
Mwandaaji wa Matukio wa TYDC Imani akitoa neno la shukurani kwa wote waliohudhulia jukwaa hilo.
Afisa Mahusiano wa TYDC Anna Emmanuel akielezea historia fupi ya umoja wao.
Mdahalo ukiwa umeanza.
Loveness Msuya akizungumzia mada inayohusu jinsi gani mtoto wa kike anaweza kusimama kwenye ndoto na malengo yake na mwisho wasiku kufanikiwa, alieleza njia na mbinu mbalimbali zinazoweza kumfikisha mtoto wa kike kule anapo pataka.
Anna Mwalongo kutoka DUCE akisisitiza kwa nguvu na kupaza sauti ya kuwasihi Mabinti kujitambua ili waweze kuepukana na vishawishi mbalimbali vinavyo sababishwa na vijana.
No comments:
Post a Comment