Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akiwaeleza wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF ikiwa ni pamoja na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) ambapo mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anaweza kujiunga na kunufaika na mafao mengi.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Hoteli ya Heritage wakiwa wanasikiliza kwa makini somo kutoka kwa Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary kuhusu mafao yatolewayo na mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage akiwa anasoma jarida kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akigawa vipeperushi na majarida yanayoelezea kwa kina huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko huo.
Wafanyakazi wa Hotel ya Heritage wakiwa wanachukua fomu kwa ajili ya kujiunga na Bima ya afya ya NHIF itolewayo kwa Bei nafuu kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
Baadhi ya watumishi wa Hoteli ya Heritage Jijini Dar es salaam wakiendelea kusoma vigezo masharti na mambo mbalimbali juu ya Bima ya afya ya NHIF inayotolewa kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
Wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage wakiendelea kupata maelezo juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS) umeendelea kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo.
Hayo yamesemwa na Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary alipokuwa akitoa maelezo na mafunzo juu ya mfuko huo na wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage iliyopo Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na kutoa maelezo juu ya mfuko huo na kutoa elimu ya juu ya mpango huo wa uchangiaji wa hiari ambapo mwanachama atatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 , atakuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake huku kiwango cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki na huduma za simu.
Bwana Hadji alisema kuwa mpango huo wa hiari unakaribisha raia na mtu asiye raia bila kusahau mjasiriamali na mfanyakazi wa serikali na kuongeza kuwa mwanachama anayejiunga katika mfuko huo huweza kupata mafao ya aina sita ambayo ni; Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali, Fao la Uzeeni, Fao la Kifo, Fao la Ugonjwa/Ulemavu, Fao la Kujitoa, na Fao la Matibabu.
Akifafanua kuhusu Fao la Matibabu, Bwana Hadji alisema kuwa kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari wanashirikiana na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo mwanachama ataweza kupatiwa huduma bure katika hospitali na maduka ya madawa yaliyosajiliwa na NHIF kote nchini.
“Mwanachama anaweza kuwasajili pia wategemezi wake watano na kuendelea kupata mafao yetu bila shida yoyote,” alisema Hadji
Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali wafanyakazi hao walionesha kufurahia unafuu wa mfuko huo na kuwataka PSPF kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wananchi wengi wajiunge kwa kuwa hupoteza fedha nyingi ambazo wangeweza kuziokoa kwa kujiunga na mfuko huo.
Aidha Hadji aliwaambia wafanyakazi hao kuwa PSPF ina wawezesha wanachama wake na jamii kwa ujumla kumiliki nyumba zilizopo Dar , Morogoro, Tabora, Mtwara, Shinyanga na Iringa ambapo wataweza kununua kwa mkopo au malipo ya mara moja pamoja na mikopo ya viwanja vilivyo sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment