Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha mloka katika mkutano wa adhara kwa lengo la kuweza kujadili changamoto mbali mbali inazowakabili
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwahutubia wananchiwa kijiji cha mloka katika mkutano wa adhara.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha mloka wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengwerwa wakati wa mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha mloka.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU) .
NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
WANANCHI wa kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Magufuli kuingilia kati haraka iwezekanavyo migogoro ya kugombania ardhi baina ya wafugaji na wakulima ya ili kuweza kuepeukana vurugu na mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kusababisha baadhi ya watu kupoteza maisha yao na uvunjifu wa amani.
Kilio hicho wamekitoa kwa mbunge wa jimbo la Rufiji wakati wa mkutano wa adhara katika kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni ulioandaliwa kwa lengo la kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabii wananchi kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Wanakijiji hao akiwemo Juma Katoto na Salum Mlanzi walisema kwamba kulingana na kukithiri kwa mapigano ya wakulima na wafugaji serikali inapaswa kulitafutua ufumbuzi suala hilo kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kufanya utaratibu wa kuipunguza mifugo iliyozidi kwani ndio chanzo cha kusababisha vurugu hizo.
Aidha katika hatua nyingne walisema kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika mashamba na kula mazao yao hali ambayo kwa sasa imesababisha kuwepo kwa njaa katika baadhi ya maeneo kutokana na kukosa chakula .
“Kwa kweli kwa sasa sisi wananchi wa kijiji hiki cha mloko bado tunakabiliwa na changamoto ya wakulima na wafugaji, maana tatio kubwa ni jamii ya wafugaji kuingiza mifugo yao katika mashamba yaetu na kua mazao yote kama vile, mahindi, mpunga, mboga mboga amabo ndizo tunategemea katika chakula, hivyo serikali inapaswa kuwachukulia hatua kali a kisheria,”alisema wananchi hao.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la rufiji Mohamed Mchengerwa ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwa kushirikiana bega kwa bega na serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu kwa ajili ya wagugaji na wakulima ili kuepukana na mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa wananchi wake.
Mchengerwa aliesma kwamba anatambua kuwepo kwa changamoto hiyo ya wafugai kuingiza migugo kiholela katika maeneo ya mashamba, lakini ameshaana kufanua jitihada hali na mali kuhakikisha kuwa serikali inatenga maeneo maalumu kwa ajili ya wakulima na wafigaji ili kuweza kuondokana na virugu amabo imekuwa ikijitokeza.
“Katika jimbo langu la rufiji kwa sasa kuna zaidi ya mifugo kama laki tatu na nusu hadi laki nne kwa hivyo kikubwa aidi hapa mii nitahakikisha kwamba vurugu hizi zinamalizika kwa kushirikiana na serikali ili kuweza kuona jinsi ya kutoa elimu kwa jamii ya wafugaji na wakulima ,ii wananachi wawee kuishi kwa amani bila ya kuwepo kwa mapigano ya aina yoyote,”alisema Mchengerwa.
WILAYA ya rufiji kwa sasa ambayo inakadiriwa kuwa na mifugo zaidi ya laki tatu na nusu bado inakabiliwa na changamoto ya migogoro ya ardhi kwa kipindi cha muda mrefu kutokana na jamii ya wakulima kuamua kuingiza mifugo yao katika maeneo ya mashamba na kula mazao hali ambayo inasababisha kuibuka kwa matukio ya mapigano na uvunjifu wa amani .
No comments:
Post a Comment