Na Genofeva Matemu –
WHUSM
Vijana nchini
wametakiwa kuiga mfano wa vijana wa Maswa Youth Family kuunganisha nguvu zao
kuibua miradi yenye tija kwani heshima ya kijana ni kujitengemea na
kulitegemeza taifa lake.
Hayo yamesema na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ufunguzi wa Kiwanda cha Chaki Jana
katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu.
“Vijana wa Maswa
Youth Family ni mfano bora wa kuigwa kwani ni vijana waliojitambua na kutambua
yakua umoja ni nguvu hivyo kuchagua fungu lililo jema na kuwa mfano bora kwa
wana Maswa na taifa kwa ujumla” alisema Mhe. Jenista.
Aidha Mhe. Jenista
amemuagiza Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kuwakopesha tena vijana wa
Maswa Youth Family shilingi milioni thelathini kutoka katika mfuko wa vijana
ili kiwanda hicho kiweze kukua kwa haraka na kuzalisha chaki kwa wingi hivyo kuweza
kuzuia soko la chaki zinazotoka nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa kiwanda cha chaki Wilayani Maswa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka amesema kuwa hadi sasa uzalishaji wa chaki unaofanywa na kiwanda
kidogo cha Maswa Youth Family unatosheleza mahitaji ya chaki kwa shule zote za
Mkoa huo na kuzipiga marufuku shule zote mkoani hapo kununua chaki nje ya Mkoa
wa Simiyu.
“Simiyu imedhamiria
kuionyesha nchi kuwa sisi ngozi nyeusi tunaweza tukaibua miradi, tukajenga
uwezo na baadaye tukazalisha kwa kuiendeleza kauli mbiu ya mkoa wetu ya bidhaa
moja wilaya moja ambayo baadaye itashuka hadi kuwa bidhaa moja kijiji kimoja na
kulifanya taifa letu kuwa taifa la viwanda” alisema Mhe. Mtaka.
Aidha Naibu Waziri
Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa Mkoa wa Simiyu umekua
wakwanza kuiishi kwa vitendo falsaga ya bidhaa moja wilaya moja na kuahidi kuiunga
mkono falsafa hiyo kujitolea kuwa balozi wa Chaki inayotengenezwa na Maswa
Youth Family ili kuweza kuitangaza nchi nzima.
Naye Mwenyekiti wa
Maswa Youth Family Bw. Kelvin Steven amesema kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa
kuzalisha chaki 38,400 kwa saa sawa na katoni 16 na iwapo uzailishaji
utafanyika kwa saa nne kiwanda kitazalisha katoni 128 kwa siku na uzalishaji
huo kwa siku 20 unategemewa kuwa katoni 2560 ambapo mahitaji kwa mwezi kwa
Wilaya inakadiriwa kuwa katoni 157 hivyo kuwa na zaidi ya katoni 2403 ambazo
zitauzwa maeneo mengine.
Mradi huu umegharimu
jumla ya shilingi 37,967,522 kati ya fedha hizo shilingi 30,967,522 ni mchango
wa Halmashauri na shilingi 70,000,000 ni mchango wa kikundi uliotokana na fedha
za mkopo waliopewa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya
watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya kuwasili katika
Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki
kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akimsikiliza
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe (aliyesimama kushoto) baada ya
kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua
kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista
Mhagama (kulia) akipokea taarifa fupi ya Wilaya ya Maswa kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe (kushoto) baada ya kuwasili katika Halmashauri
hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa
na vijana wa Maswa Youth Family.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza na
viongozi kutoka Mkoa wa Simiyu na Halmashauri ya Maswa baada ya kuwasili katika
Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki
kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (wapili kulia) akiwasili
katika kiwanda cha chaki kijulikanacho kwa jina la Maswa Youth Family jana
katika Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu kwa ajili ya kukizindua kiwanda hicho
rasmi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na watatu kulia ni
Mwenyekiti wa kiwanda hicho Bw. Kelvin Steven.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista
Mhagama (watatu kulia) akipata taarifa fupi ya kiwanda cha Maswa Youth Family
kutoka kwa Mwenyekiti wa kiwanda hicho Bw. Kelvin Steven (kulia) baada ya
kuwasili katika kiwanda hicho kwa ajili ya kukizindua rasmi jana katika
Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu. Wapili kulia ni Naibu Waziri Kazi, Ajira na
Vijana Mhe. Antony Mavunde na kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akimimina mchanganyiko
wa mahitaji ulioandaliwa kwa ajili ya kutengeneza chaki katika moja ya mashine
ya kutengeneza
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista
Mhagama (katikati) akiangalia chaki zilizotengenezwa katika kiwanda cha Maswa
Youth Family kabla ya kukizundua rasmi kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya
Maswa Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka na kulia ni kijana kutoka Maswa Youth Family Bw. Razaro Zabroni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) kwa
kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Mkuu wa
Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe (kushoto) kukata utepe kuzindua rasmi
kiwanda cha chaki cha Maswa Youth Family
jana katika Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony
Mavunde akizungumza na vijana wa Maswa Youth Family pamoja na wananchi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya uzinduzi wa kiwanda cha chaki jana
katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus
Kamani
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
akizungumza na vijana wa Maswa Youth Family pamoja na wananchi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Maswa baada ya uzinduzi wa kiwanda cha chaki jana katika
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista
Mhagama (aliyesimama) akizungumza na vijana wa Maswa Youth Family pamoja na
wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya kuzinduzi wa kiwanda cha
chaki jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu. Kulia ni Naibu
Waziri Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu
Dkt. Titus Kamani
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) baada ya
kukizindua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family
jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja
na vijana wa Maswa Youth Family na baadhi ya viongozi waliojumuika naye
katika uzinduzi wa kiwanda cha chaki jana katika Halmashauri ya Wilaya
ya Maswa Mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment