Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akiwasilisha mada ya masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa
mkutano wa wadau wa masuala hayo walipowasilisha Matokeo ya Tafiti Mpya
ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini uliofanyika katika
Ukumbi wa mikutano hoteli ya Serena Dar es Salaam Oktoba 12, 2016.(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkalimani
wa lugha ya alama Bw.Thomas Shayo akifasiri ujumbe kwa kundi la watu
wenye ulemavu (wasiosikia) uliotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani)
wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum
uliofanyika katika Ukiumbi wa hoteli ya Serena Dar es Salaam. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mtafiti
Rika Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Bi. Regina Mbaji akiwasilisha
mada wakati mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum
walipowasilisha matokeo ya tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya
Ulemavu na Uzee Nchini Ukumbi wa Mikutano hoteli ya Serena Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mshiriki
Rika (kundi la wazee) Bi.Elizabeth Nkwera akitoa mada ya usawa wa
huduma za kijamii kwa makundi maalum wakati wa Mkutano wa wadau wa
masuala la watu wenye mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya tafiti
Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akizungumza na baadhi ya wadau walioshiriki katika Mkutano wa
kujadili masuala ya watu wenye mahitaji maalum uliofanyika katika hoteli
ya Serena Oktoba 12, 2016, wa kwanza kulia ni Bi. Clotilda Isdori na
katikati ni Bw.Elisha Sibale. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah
Possi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa
Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum ulioandaliwa
na Mashirika ya misaada. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment