MAHAKAMA
Kuu Tanzania, Divisheni ya Ardhi, imetupilia mbali maombi ya Kampuni ya Mbowe
Hotels Limited inayomikiwa na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mhe Freeman Mbowe ya kutaka kurudishwa kwenye jengo la
Billicanas kwa sababu waliondolewa katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) kwa kufuata taratibu zote za kisheria.
Aidha,
Jaji Sivangilwa Mwangesi alisema shirika hilo lilifuata taratibu zote kumwondoa
mlalamikaji katika jengo hilo na kwamba inashikilia mali zake kihalali hadi
atakapolipa kodi ya Sh.Bilioni 1.3 kama anavyodaiwa.
Akisoma
uamuzi huo mapema jana Jaji Mwangesi baada ya kusikiliza hoja za pande zote
mbili, mahakama yake iliamua kutupilia mbali maombi hayo yaliyofunguliwa chini
ya hati ya dharula bila kulipwa gharama.
Jaji
alisema madai ya mlalamikaji kwamba aliondolewa kinyume cha sheria katika jengo
hilo na kampuni ya udalali isiyosajiliwa hayana mashiko kisheria mahakama
inafutilia mbali kesi hiyo.
“Mahakama
hii baada ya kupitia hoja za pande zote mbili imeona kwamba mlalamikiwa wa
kwanza NHC alifuata taratibu zote kumtoa mlalamikaji katika jengo hilo … pia
imeona kwamba kampuni ya udalali Foster Auctioneers and General Traders
ilifanyakazi ya kuondoa mali zake kihali, inatupilia maombi haya bila kulipwa
gharama ya kesi hii” alisema Jaji Mwangesi.
Aidha
akifafanua zaidi jaji alisema pamoja na madai ya kuwepo kwa mkataba kati ya NHC
na Mbowe, mkataba huo haukuwahi kutekelezwa kwa hiyo ni sawa na kwamba
haupo.Upande wa mlalamikaji uliongozwa na Mawakili Peter Kibatala akisaidiana
na John Mallya.
Upande
wa walalamikaji uliongozwa na Mawakili Aloyce Sekule, Aliko Mwamanenge na
Mariam Mungura.Wakili Mwamanenge akizungumza na Globu ya Jamii nje ya viunga
vya mahakama hiyo, alisema mlalamikaji alisema mahakama imetenda haki na kwamba
mlalamikaji alidai kuwa na mkataba kati yake na NHC, lakini mahakama hiyo imeona
mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.
“Mahakama
imeona dalali alifanya kazi yake kwa kufuata taratibu za kisheria na hata hizo
mali zinashikiliwa na mteja kihalali hadi atakapolipa deni la Sh. Bilini 1.3
ndipo atarejeshewa mali hizo” alisema wakili Mwamanenge.
Kwa
upande wake Wakili Mallya alisema wamewasilisha maombi ya kuomba nakala ya
uamuzi ili waombe marejeo Mahakama ya Rufani Tanzania.
Pia,
wamepeleka maombi ya kuomba chochote kisifanyike katika jengo hilo na kuhusu
mali za Mbowe mpaka uamuzi utakapotolewa na Mahakama ya Rufani dhidi ya
maombi yao ya marejeo.
Alisema
Jaji katika uamuzi wake amesema mkataba kati ya NHC na Mbowe haukuwahi
kutekelezwa na haupo kisheria kwa hiyo tunasubiri nakala ya uamuzi tuupitie ili
tuwasilishe maombi ya marejeo mahakama ya juu” alisema Wakili Mallya.
Maombi
hayo yaliyosajiliwa mahakamani hapo kwa namba 722 ya 2016 dhidi ya NHC,
yalifunguliwa chini ya hati ya dharula baada ya Mbowe kuondolewa kwenye jengo
hilo mapema Septemba Mosi, mwaka huu.
Katika
hati ya kiapo Mbowe alidai kwamba yeye na mlalamikaji katika mgogoro huo
warejee kwenye usuluhishi kwa mujibu wa mkataba wa ubia huo.
Hata
hivyo, upande wa walalamikiwa ulipinga hatua hiyo kutokana na kutokuwepo kwa
nyaraka hizo mahakamani hapo juu ya mwenendo wa mchakato huo wa usuluhishi,
kwani walitoa ilani ya kumhamisha Mbowe katika jengo hilo kwa kufuata sheria.
Pia
ilidaiwa kuwa Mbowe katika jengo hilo ni mpangaji na hata mkataba wa
ushirikiano unaodaiwa umefanyika kati yao kwa sasa hauwezi kufanyakazi kwa kuwa
ulishakwisha muda wake.Katika madai ya msingi Mbowe alidai kuwa si mpangaji
katika jengo hilo, bali ni mmbia ambaye anamiliki asilimia 75 katika uendeshaji
wake huku NHC wakimiliki asilimia 25.
Hoja
nyingine alidai kuwa, hata kama angekuwa anadaiwa kodi kama wanavyodai NHC,
kuondolewa kwake kulifanywa bila kuzingatia sheria kwani hakukuwa na amri ya
mahakama inayowapa walalamikiwa nguvu ya kisheria ya kumwondoa.
Kwa
upande mwingine, Mbowe kupitia hati ya kiapo alisema hadaiwi hata senti tano na
NHC kama pango la jengo la Billcanas, na kwamba amekuwa akilipa tozo zote
zinazotakiwa kwa mujibu wa mkataba baina yake na shirika hilo.
Kwa
mujibu wa hati ya kiapo aliyoiwasilisha mahakamani, mmiliki huyo wa Kampuni ya
Mbowe Hotels Ltd alidai kwa mujibu wa mkataba wa ubia wa pande hizo mbili,
anapaswa kuwalipa NHC mapato ya jengo kila mwezi.
Katika
hati hiyo, Mbowe alisema hadaiwi fedha yoyote kwani amekuwa akitekeleza matakwa
hayo ya kimkataba kama yalivyosainiwa mwaka 1997, huku akiambatanisha ushahidi
wa risiti ya fedha ambazo amekuwa akilipa.
No comments:
Post a Comment