Muonekano
wa kivuko kipya cha MV Kazi kikiwa katika hatua za awali za ujenzi
wake. Kivuko hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Watendaji wa Kampuni ya Songoro wanaojenga kivuko kipya
cha MV. Kazi, kinachojengwa katika yadi ya Bandari jijini Dar es Salaam,
mara baada ya kutembelea na kujionea ujenzi wake. Kivuko hicho kipya
kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
akiongea na mafundi wa wa Kampuni ya Songoro wanaojenga kivuko kipya cha
MV. Kazi, kinachojengwa katika yadi ya Bandari jijini Dar es Salaam,
mara baada ya kutembelea na kujionea ujenzi wake. Kivuko hicho kipya
kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA),
alipotembelea eneo la Kivukoni. Katikati ni Mkuu wa Kivuko upande wa Dar
es Salaam, Eng. Lukombe King’ombe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiongea na
mwanafunzi Arafat Kondo wakati alipotembelea kivuko cha MV. Kigamboni
kujionea utendaji wake.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akishuka
kwenye pantoni mara baada ya kukagua utendaji wa kivuko cha MV.
Kigamboni.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisikiliza
taarifa ya matumizi ya mafuta kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Ufundi na
Umeme nchini (TEMESA) alipotembelea kivuko cha MV. Kigamboni.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
WAZIRI
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza
uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha
wanaweka mipango madhubuti ya kuongeza mapato katika vivuko vya MV.
Kigamboni na MV. Magogoni kutoka Shilingi Milioni 14 ambazo zinakusanywa
hivi sasa hadi kufikia Milioni 19 kwa siku.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua vivuko hivyo na kuongea na
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu Prof. Mbarawa amesema kuwa
kipimo cha utendaji huo utafanyika ndani ya miezi minne ili kuongeza
ufanisi katika utendaji kazi wa vivuko hivyo na kuweza kufikia malengo.
“Hatushindwi
kutafuta mtu mwingine mwenye ujuzi na utendaji wa kazi uliotukuka, kama
lengo la kukusanya milioni 19 halitafikiwa mkuu wa kivuko atafute kazi
nyingine na tutafanya hivyo mpaka tuhakikishe tunapata atayeweza
kukusanya kiwango hiki”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa ameutaka Wakala huo kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato
katika vivuko hivyo na kuwa wa kieletroniki ili kudhibiti ubadhilifu
unaofanywa na watumishi wasio waaminifu wakati wa utoaji huduma.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amejionea maendeleo ya ujenzi wa kivuko
kipya cha MV. Kazi nakusema kuwa kivuko hicho kitarahisisha usafiri kwa
wakazi wa Kigamboni.
Aidha,
amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport kumaliza
utengenezaji wa kivuko hicho ifikapo Mwezi Disemba mwaka huu ili
watanzania wapate huduma bora za usafiri.
Ameongeza
kuwa Kampuni hiyo ihakikishe kuwa inasimamia upatikanaji wa injini za
Kivuko hicho kwa wakati ili kusaidia ujenzi huo kukamilika kwa muda
uliopangwa.
“Nina
imani na kasi mnayokwenda nayo, na nina uhakika Kivuko hiki kitamalizika
kwa wakati naomba muwe waangalifu na kuhakikisha kwamba injini za
kivuko hiki zinawasili mapema”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye
Mkurugenzi wa Karakana ya Dar es Salaam wa Kampuni ya Songoro Marine,
Major Saleh Songoro amesema kuwa ujenzi wa Kivuko cha MV Kazi upo katika
hatua nzuri ambapo kwa sasa wanakamilisha kazi ya kuchomea milango
katika kivuko hicho.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mgwatu amemuhakikishia Waziri
Prof. Mbarawa kuwa maagizo yote yatatekelezwa ikiwemo kutatua changamoto
mbalimbali zinazokabili Wakala huo.
Dkt.
Mgwatu amewataka wananchi kuwa na subira wakati kivuko cha MV. Kazi
kinamalizika kujengwa kwani itapunguza kama sio kuondoa msongamano
uliopo sasa katika maeneo ya Magogoni na Kigamboni.
Ujenzi
wa kivuko cha MV Kazi ulianza Mwezi Juni mwaka huu ambapo kina uwezo wa
kubeba tani 170 sawa na watu 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment