Thursday, October 20, 2016

SHULE YA SEKONDARI YA MALANGALI YAPATA NEEMA KUTOKA KWA MALANGALI ALUMNI ASSOCIATION (MAAS)


Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania

mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Malangali na kuwaeleza jinsi gani shule hiyo ilivyowapa mafanikio hadi sasa walipofikia.  


Na Fredy Mgunda,Iringa


Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamewataka vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali walinufaika na elimu kutoka shule ya malangali kurudisha fadhila katika shule hiyo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) alisema kuwa maendeleo aliyoyapata sasa ni kutoka na shule ya mangali hivyo ameamua kurudi na kuisadia shule hiyo. 

“Wafanyakazi na viongozi mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania.” Alisema Kevela.Kevela amesema kuwa shule nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbli zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule walizosoma.

Naye Padre wa kanisa la kikatoriki mkoani mbeya Telesipholi Tweve aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.

“Leo nimerudi katika shule hii ya malangali kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi kama MAAS tumeanza kwa kukarabati ukumbi ambao utakuwa na faida kwao kwa kutumia kwenye sherehe na kukodishwa pia”.alisema Tweve

Kwa upande wake mwenyekiti wa Malangali Alumni association (MAAS) Paul Mng’ong’o alisema kuwa wameanza kuisaidia shule ya Malangali muda mrefu kwa kuwa tayari wameshakarabati ukumbi wa shule,wamewanunulia tv na king’amuzi kwa ajili ya habari na wanaendelea kutatua matatizo ya shule hiyo.

“Hebu angalia sisi tuliosoma hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado ipo pale pale na inazidi kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili kurudisha fadhila kwa kuwa wengi wetu tumepata mafanikio makubwa kutoka shule hii,tunaviongozi wengi,matajili wengi ,wakulima wakubwa sana hapa nchini wote wamesoma katika shule hii”.Alisema Mng’ong’o

Lakini pia Mng’ong’o alisema kuwa lengo la kundi la Malangali Alumni Association kuunganisha wanafunzi wote waliowahi kusoma shule ya secondary ya Malangali na kuweza kupeana malengo na kusaidiana pale wanapokwama kimalengo.


Shule ya Malangali ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali,taasisiza Umma na sekta walijengewa msingi wa kwanza wa maisha.kaika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake.

No comments:

Post a Comment