Rais Dkt John Magufuli
Wahitimu Aziza Mkawa na Amina Ally wakimlisha keki mwenzao Eugenia Msahala aliyehitimu jana chuo kikuu cha Iringa
Wahitimu wa chuo kikuu cha Iringa Rubeny Nyagawa kulia ,Anna Laiza , Deodatus Mnyang'ari na Anna Lwanda wakijipongeza kwa keki baada ya kuhitimu digirii ya biashara na utawala katika chuo kikuu cha Iringa
Na MatukiodaimaBlog
UONGOZI wa Chuo kikuu cha Iringa (UoI) umepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli juu ya uhakiki wa watumishi hewa wenye vyeti feki kwa madai hatua hiyo ni nzuri itasaidia kupata wataalam wenye sifa sahihi tofauti na ilivyokuwa awali kuwa na utitiri wa watumishi wasio na uwezo.
Pongezi hizo zimetolewa jana wakati wa mahafali ya chuo hicho na mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, askafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Odenburg Mdegela alisema kuwa zoezi hilo linapembua mchele na chuya na kuwaacha wale wenye vyeti halai tu.
Alisema ilikuwa si sahihi mmoja akae darasani miaka mitatu na mwingine apate cheti kutoka kariakoo tena kikiwa a ufaulu wa juu kuliko Yule aliyekaa darasani.
Dkt. Mdegela alisema watu hawa wanapokutana kazini Yule alipata vyeti bandia vyenye ufaulu wa hali ya juu anakuwa hajui kazi jambo lililokuwa likirudisha nyuma maendeleo ya taasisi nyingi na nchi kwa ujumla.
“Uhakiki wa vyeti unapaswa kuungwa mkono na wadau wote wakiwemo wa elimu kwa kuwa hali ilikuwa mbaya huku wale wenye vyeti badia vikiwa na ufaulu wa hali ya juu ilhali hawajui kazi”, alisema Dkt. Mdegela
Aidha alisema Chuo hicho kinajipanga kuachana na mtazamo uliojengeka kwa muda mrefu wa kujiendesha kwa kutegemea wafadhili mbalimbali wa ndani na nje ya nchi pamoja na mikopo ya ada za wanafunzi kutoka serikalini.
Alisema wanatarajia kuanzisha Asasi itakayokuwa imeungwanishwa na Chuo ambayp itakuwa ikitoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi ambao wamekwama kupata huduma hiyo kutoka maeneo mengine.
Kwa upande wake mkuu wa Chuo hicho, Jaji mkuu mstaafu Augustine Ramadhani alisema ni vema wahitimu wakawa wazalendo kwa nchi yao na kuitumia elimu waliyoipata kwa maendeleo ya watanzania wote.
Huku makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Joseph Madumula alisema mazingira ya utoaji wa elimu kwa sasa yamekuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na Chuo kikuu kimoja cha Dar es Salaam kikiwa na matawi mawili ya Sokoine na Muhimbili.
Aliongeza kuwa kwa sasa kuna zaidi ya vyuo vikuu 60 vya binafsi na serikali lakini idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa haijaongezeka kulingana na vyuo idadi ya vyuo.
No comments:
Post a Comment