Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) Andrew Ngobole akizungumza katika Mahafali ya Chuo hicho ambapo Wanafunzi wametunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada.Picha na Frednand Shayo. |
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akikabidhiwa Zawadi na Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC) Joseph Mayagila katika Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.Picha na Frednand Shayo. Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC) Joseph Mayagila akizungumza katika Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo,wapili kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro,wakwanza kushoto ni Diwani wa kata ya Themi ,Melans Kinabo na kulia ni Mkurugenzi wa Safina Radio Elifuraha Samboto Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akimtunuku cheti cha stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji Amani Mmbando wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC),wawatu kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC) Joseph Mayagila Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akimtunuku cheti cha stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji Editha Makundi wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC),wawatu kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC) Joseph Mayagila. picha ya pamoja na wahitimu |
Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro akizungumza katika Mahafali ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) ,Kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho Joseph Mayagila,kushoto ni Diwani wa kata ya Themi ,Melans Kinabo. |
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wafanyakazi wa CHUO |
Wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) wakirusha kofia juu ishara ya kuonyesha kutunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada. Na.Vero Ignatus,Arusha.
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amewatunuku zaidi ya wahitimu 50 waliohitimu katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji (AJTC) huku akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za jamii na kuleta mabadiliko kupitia kalamu zao.
Kalisti amewataka Wanahabari kujikita katika kuandika habari za kijamii zitakazosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuleta suluhu kwenye matatizo ya jamii.
Ameishauri serikali kuangalia upya mswada wa habari na kuufanyia marekebisho katika vipengelea ambavyo vinaminya haki ya habari.
Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji ,Joseph Mayagila amesema kuwa tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika kuchochea maendeleo ya nchi kwani bila taarifa hakuna maendeleo.
Alisema kuwa ni vyema serikali ikatazama upya utekelezaji wa sheria mpya na kufanyia kazi mapungufu ili wanahabari waendelee kuwahabarisha Watanzania.
|
No comments:
Post a Comment