Naibu
waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura,
akitoa hotuba ya ufunguzi wa chilumbo, (kongamano) la Kiswahili,
lililofadhiliwa na benki ya MCB, na kufanyika chuo cha kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2017.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI
ya Mwalimu, (MCB), imetoa semina kwa walimu na washiriki wa Chilumbo,
(Kongamano), la Kiswahili lililofanyika Chuo Cha Mwalimu Nyerere Kigamboni
jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2017.
Katika
semina hiyo, maafisa wa MCB walielezea huduma mbalimbali zitolewazo na benki
hiyo mpya inayomilikiwa na chama cha walimu nchini, (TTU), ambapo Meneja
Mahusiano ya wateja wa benki hiyo, Bw.Charles Shadrack, (pichani juu), alisema, benki hiyo
inatoa huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu.
“Kwa
mfanyakazi wa serikali, anachotakiwa kuja nacho baada ya kufungua akaunti
kwenye benki yetu ni Salary sleep ambapo tunatoa mkopo wa hadi shilingi milioni
30.” Alisema.
Alisema,
benki hiyo pia imo kwenye kundi la mabenki yanayotumia ATM za umoja hivyo mteja
anayo fursa ya kupata huduma za kibenki mahala popote nchini.
Akifungua
chilumbo hilo, Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.
Anastazuia Wambura, amewataka washiriki kukienzi Kiswahili kwani ni lugha
inayokua kwa kasi duniani.
“Rais
wetu ameonyesha njia, niwape changamoto magwiji wa Kiswahili, jifunzeni kwa
bidii ili mkitumie kama ajira kwani soko la walimu wa Kiswahili linapanuka siku
hadi siku.” Aisema.
Wasiriki wakifurahia mada zilizokuwa zikitolewa
Washiriki wakiwa kwenye ukumbi wa Utamaduni palikofanyika chilumbo
Naibu
waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura,
(kushoto), akipena mikono na Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Bi. Rahma
Ngassa, mara baada ya kutoa hotuba yake
Meneja
Masoko na Uhusiano wa MCB, Rahma Ngassa, Meneja wa Huduma kwa wateja wa
benki hiyo, Bi.Flora Mbogo na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles
Shadrack, wakiwasikiliza washiriki mbalimbali waliohudhuria chilumbo
(kongamano), hilo na wakataka kujua huduma zitolewazo na MCB
Meneja
Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack,(kushoto), akifafanua jambo kwa
washiriki hawa waliokuwa na kiu ya kujua huduma zitolewazo na benki
hiyo mpya kabisa hapa nchini
Meneja
wa MCB, tawi la Samora katikati ya jiji, Bw.Cassian Clovis, (kushoto),
akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, na
Afisa Mikopo wa benki hiyo, Bw.Isaya Hagamu, huku chilumbo kikiendelea
Wimbo wa taifa ukiimbwa
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, anayeshughulikia
masuala ya Mipango, Fedha na Utawala, Dkt.Magreth Shiwa, akitoa hotuba
ya kuwakaribisha wageni
Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki hiyo. |
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba |
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini
Msanii Muhogo mchungu naye alikuwepo kwenye chilumbo (kongamano) la Kiswahili
Afisa
Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, (wakwanza kushoto), akitoa
maelezo ya shughuli zifanywazo na benki hiyo kwa washiriki hawa
waliokuwa na hamu ya kutaka kujua huduma zitolewazo na benki hyo
Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki hiyo.
Mtunzi maarufu wa vitabu Shafi Adam Shafi naye alikuwepo
Meneja
Masoko na Uhusioano wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, (katikati), na Meneja
Uhusiano wa wateja, Bw. Charles Shadrack, (kushoto), wakimsikiliza
mwenyeji wao Meneja Uhusioano wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,
Bi. Evelyn Mpasha
No comments:
Post a Comment