Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Christina Mdeme akizungumza na wakazi wa Kata
ya Nala alipowatembelea na kusikiliza maoni na changamoto mbalimbali
zilizopo katika kuanza kutekelaza radi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa
Kimataifa Dodoma. (Picha zote na Raymond Mushumbusi - WHUSM Dodoma)
Diwani
wa Kata ya Nala Mhe. Brayceon Leonard Eliah akiwasisitiza wakazi wa
Kata yake kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kutekeleza mradi huu wa
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Dodoma Bw. Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme(hayupo pichani) katika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.
Afisa
Mipango Miji Manispaa ya Dodoma Bw. Clemence Msuva akieleza taratibu za
tathimini ya eneo lililopo katika Kata ya Nala utakapojengwa uwanja wa
Michezo wa Kimataifa zitavyofanyika ili kuwezesha mradi huo kuanza
mapema.
Mmoja
wa Mkazi wa kata ya Nala Stanley Wilson akiuliza swali kwa Kamati Ndogo
ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa
kuhusu utekelzaji wa mradi huo na faida watakazopata wakazi wa kata ya
Nala na Dodoma kwa ujumla.
Mwanasheria
kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bw. Evordy Kyando
akiwahakikishia wakazi wa Kata ya Nala kuwa Sheria na Taratibu
zitafuatwa katika ulipaji wa fidia kwao. Baadhi ya wakazi wa kata ya Nala wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme(Hayupo Pichani) alipowatembelea na kusikiliza hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Nala wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme(Hayupo Pichani) alipowatembelea na kusikiliza hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
MKUU
wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme amewatahadharisha wakazi wa
Kata ya Nala watakaofanya aina yoyote ya udanganyifu katika ulipaji
fidia kwao kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa
Kimataifa utaojengwa Mjini Dodoma.
Ameyasema
hayo wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nala
alipowatembelea na kusikiliza hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa
wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.
“Wewe
kama unajijua sio mkazi halali wa eneo unapopita mradi huu naomba
ukafute jina lako ila tukikubaini tutakuchukulia hatua kali za kisheria”
alisisitiza Mhe. Christina.
Mhe.
Christina Mdeme ameongeza kuwa Serikali haipo tayari kupoteza hela kwa
ajili ya kulipa watu wasiostahili katika mradi huo na kwamba kila anayehusika kulipwa fidia kihalali atalipwa.
Aidha
Mhe. Christina Mdeme amewahakikishia wakazi wa Kata ya Nala kuwa
Serikali haitamdhulumu mtu yoyote na atahakikisha kila anayepaswa
kulipwa fidia analipwa fidia anayostahili.
Pia
amewatahadharisha wakazi hao kutotumiwa na viongozi au vikundi vya watu
kwa manufaa ya kujipatia pesa zinazotokana na fidia za mradi huo kwa
njia za udanganyifu.
Kwa
upande wake Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Bw. Evordy Kyando amewaomba wakazi wa Kata ya Nala kuwa watulivu
na kwamba Sheria na Taratibu za ulipaji fidia zitafuatwa kikamilifu
katika zoezi hilo.
Akitoa
maelezo ya kwa niaba ya Kamati ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa
Uwanja wa Michezo wa Kimatafa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw.Salum Mkuya
amewahikikishia wakazi wa Kata ya Nala ushirikiano kutoka kwa Kamati
yake ili kufanikisha mradi huu wa kimataifa.
No comments:
Post a Comment