Meneja
wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Sylvia Meku (katikati) akiwa na wadau wakionesha kitabu cha uwiano wa
takwimu za wanawake na wanaume wakati wa hafla ya kuzindua kitabu hicho
iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids),
Jumanne Issango, Ofisa wa Takwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger,
Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda na Mwanahabari Philip..Kitabu hicho
kimeandikwa na wanafunzi watano kutoka Tanzania waliopata mafunzo ya
miezi 11 nchini Sweden.
Mada kuhusu mafunzo hayo zikitolewa kabla ya uzinduzi.
Wafadhili wa mafunzo hayo kutoka nchini Sweden wakifuatilia mada kuhusu mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango (kushoto) na Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa karibu hafla hiyo.
Mtakwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda akichangia jambo
Mada zikiendelea kutolewa.
Mhadhiri
kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki
(kushoto), akizungumzia mafunzo ya takwimu waliopata nchini Sweden.
Mratibu wa masuala ya Jinsia wa Tacaids, Jacob Kayombo akichangia jambo katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tacaids, Jerome Kamwela akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina akichangia.
Washiriki wa mafunzo hayo (walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa. Kutoka kulia Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina, Mhadhiri
kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki, Ofisa wa
Jinsia wa Tacaids, Judith Luande, Philbert Mrema kutoka NBS na Mariam
Kitembe kutoka NBS.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
WANAUME wameonekana kuwa wengi katika nafasi mbalimbali ukilinganisha na wanawake.
Hayo
yamebainishwa na Mhadhiri wa Chuo cha Takwimu Afrika Mashariki, Chisker
Masaki wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Uwiano wa Taarifa za Takwimu kwa
Wanawake na Wanaume Tanzania.
Alisema
kitabu hicho kimeandaliwa na washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji wa
taarifa za takwimu kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Hakielimu ,
Ofisi yaTaifa ya Takwimu (NBS) na Chuo cha Takwimu cha AfrikaMashariki,
chini ya wakufunzi wa masuala ya ukusanyaji wa taarifa kutoka nchini
Sweden.
Masaki
alisema utafiti unaonesha kuwa kuna tofauti kubwa za uwiano kati
ya mwanamke na mwaume katika nyanja za kimaendeleo na kijamii, ambapo
maeneo mengi yanaonekana kutwaliwa na wanaume kuliko wanawake.
Akitolea
mfano upande wa elimu kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu
wasichana wanaoandikishwa hadi kufikia chuo kikuu ni wachache
ukilinganisha na wavulana, watu wenye nafasi nzuri maofisini hasa
ngazi za Ukurugenzi na mameneja wengi ni wanaume ukilinganisha na
wanawake,viongozi wa kisiasa mfano mawaziri na wabunge wanawake ni
wachache ukilinganisha na wanaume.
Alisema
pamoja na uwiano huo wa wanaume kuwa kiwango kikubwa katika masuala ya
maendeleo wanawake wamekuwa wakichukua nafasi kubwa katika kuathirika
na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Mafunzo
hayo ya ukusanyaji wa taarifa yalianza tangu mwaka 2016 mwezi Mei hadi
Machi 2017 ambapo mafunzo yalifanyika nchini Sweden ni ukusanyaji wa
taarifa pamoja na uandaaji wake kitabu ukafanyika Tanzania. (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment