Thursday, April 20, 2017

China yasema inahofia vitisho vya nyuklia vya Korea Kaskazini

Pyongyang (KCNA) - 16 ApriliHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNorth Korea ilionyesha uwezo wake wa kivita wakati wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il-sung's birth
China imesema kuwa ina waswasi mkubwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ,kufuatia mahojiano ya afisa mmoja wa taifa hilo na BBC.
Naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini aliambia BBC kwamba Pyongyang itaendelea kuyafanyia majaribio makombora yake na itarusha bomu la nuklia ikibaini kwamba Marekani inataka kuishambulia.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lu Kang amesema kuwa China ilipinga vitendo ama matamshi ambayo huenda yakasababisha hali zaidi ya wasiwasi.
Kumekuwa na matamshi ya chuki kutoka kwa pande zote mbili katika siku za hivi karibuni.
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ambaye amekuwa akitembelea eneo hilo ameonya Korea Kaskazini kutoijaribu Marekani na kusema kuwa wakati wa subira dhidi ya Pyongyang umekwisha.
Mwandishi wa BBC Stephen McDonnel mjini Beijing anasema kuwa serikali ya China inaonekana kukerwa na Korea Kaskazini ambaye mwandani wake.
''Nimeona ripoti ya hivi karibuni," Bw Lu alisema kuhusu mahojiano hayo ya BBC.
''China ina wasiwasi mkubwa kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini na utengenezaji wa silaha''.
China inaunga mkono mpango wote wa kusitisha uundaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea, kuimarisha amani na uthabiti katika rais ya Korea mbali na kuendelea kutatua maswala tofauti kupitia mazungumzo na majadiliano.
Korea Kaskazini ilifanya maonyesho ya gwaride la kijeshi wikendi iliopita na kujaribu kombora jingine siku ya Jumapili ambalo Pentagon inasema lililipuka muda tu liliporushwa.
Pyongyang imesema kuwa itafanyia majaribio makombora yake kila wiki na kuonya vita vikubwa iwapo Marekani itaishambulia.
Iwapo Marekani inapanga shambulio la kijeshi dhidi yetu,tutalipiza kwa shambulio la kinyuklia kwa kutumia mbinu yetu, alisema naibu wa waziri wa maswala ya kigeni Song-ryol siku ya Jumatatu.
USS Carl Vinson Picha: 14 Aprili 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya kubeba ndege za kivita ya USS Carl Vinson (kushoto) na meli nyingine zilielekea Bahari ya Hindi
Baadaye bwana Pence aliapa kulishinda shambulio lolote na kukabiliana na utumizi wowote wa silaha za kisasa ambapo zile za nyuklia kwa kujibu na shambulio kubwa.
Meli ya wanamaji wa marekani ya Carl Vinson inayobeba ndege za kijeshi pamoja na meli za kijeshi, inaelekea katika bahari ya magharibi mwa Pasifiki kulingana na kamanda wa eneo hilo kufuatia agizo la rais donald Trump wiki iliopita.
Imebainika kwamba wakati agizo hilo lilipotolewa meli hiyo ilikuwa ikielekea upande tofauti.
Haijulikani iwapo hatua hiyo ilifanywa kimakusudi, ni mabadiliko ya kimkakati ama mawasiliano mabaya kulingana na mwandishi wa BBC nchini Korea Stephens Evans.
North Korean missile range


No comments:

Post a Comment