Thursday, April 13, 2017

Marekani yawawekea vikwazo wababe wa kivita CAR

Mpiganaji nchini CARHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMpiganaji nchini CAR
Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo vya kifedha viongozi wawili wa makundi ya wanamgambo wanaotuhumiwa kuchochea mzozo katika jamuhuri ya Afrika ya kati CAR
Vikwazo dhidi ya wawili hao wanaotoka katika pande pinzani katika mzozo huo, ni miongoni ya mikakati ya Marekani ya kukabiliana na mgogoro katika taifa hilo, kulingana na taarifa kutoka wizara ya fedha Marekani.
Mali zozote walizonazo nchini Marekani zitapigwa tanji, taarifa hiyo imeongezea.
CAR imekabiliwa na mzozo wa kikabila pamoja na ule wa kidini tangu 2013.
Wizara ya fedha nchini Marekani imesema kwamba raia wa taifa hilo watazuiliwa kushiriki kibiashara na Abdoulaye Hissene na Maxime Mokom.
Bwana Hissene ni kiongozi wa waasi wa kiislamu wa kundi la Seleka naye Bwana Mokom akiwa kiongozi wa kundi kubwa kikristo la anti-Balaka
Maelfu ya watu wameuwawa huku idadi kubwa ya raia wakiwachwa bila makao katika kipindi cha miaka minne ya mzozo huo.

Kundi la Seleka lilishikilia mamlaka kwa muda mwezi Machi 2013 na kumng'atua mamlakani rais mkristo Francois Bozize.
Waasi hao baadaye walitimuliwa na kusababisha ghasia dhidi ya waislamu walio wachache hatua iliyochukuliwa na wapiganaji wa kundi la kikristo la anti-Balaka

No comments:

Post a Comment