Tuesday, May 2, 2017

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Mei 3, 2017) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Mei 3, 2017) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yatakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha uandishi wa habari Zanzibar Kilimani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo Shifaa Saidi Hassan kwa vyombo vya habari, imesema maadhimisho ya mwaka huu yameandaliwa kwa pamoja na taasisi nne za habari kwa lengo la kuimarisha umoja miongoni mwao na kutilia mkazo ujumbe wa mwaka huu uliotolewa na umoja wa mataifa.

Shifaa amezitaja baadhi ya shughuli zitakazofanyika wakati wa maadhimisho hayo kuwa pamoja na hutuba ya mgeni rasmi, pia mada mbali mbali zitawasilishwa na kujadiliwa na washiriki wa kongamano hilo ili wadau wa sekta hiyo waweze kutathmini utendaji wa vyombo vya habari, mafanikio yaliyopatikana na changamoto zinazoikabili tasnia ya habari nchini.

Ameeleza kuwa Katika maadhimisho ya mwaka huu yataadhimishwa kwa mashirikioano ya taasisi nne za kihabari ambazo ni Baraza la habari Tanzania – MCT),  Klabu ya waandishi wa habari Zanzibar  (ZPC), Chuo cha uandishi wa habari Zanzibar na TAMWA (chama cha wanahabari wanawake Tanzania).

Amefafanua kwamba lengo la kuadhimisha siku hiyo kwa pamoja ni  kukuza mashirikiano kati ya taasisi hizo  kama inavyohimizwa na ujumbe wa mwaka huu.

 Ofisa huyo amesema kauli mbiu ya siku hiyo kuwa ni “ umakini wa fikra, kwa wakati muhimu; nafasi ya vyombo vya habari katika kuendeleza amani, haki na ujumuishwaji inawakumbusha wanahabari na wadau wa sekta hiyo kuzingatia maadili na misingi ya taaluma yao katika utendaji wa kazi zao”.

Siku ya uhuru wa habari ulimwenguni huadhimimishwa kila ifikapo Mei 3 kila mwaka kwa lengo la kuongeza uelewa na umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari kwa jamii na kuzikumbusha serikali za mataifa wananchama wa umoja wa mataifa wajibu wa kuheshimu, kustawisha na kutekeleza haki ya uhuru wa kujieleza katika mataifa yao.

No comments:

Post a Comment