Monday, October 16, 2017

TATIZO LA UMEME MTWARA NA LINDI KUPATIWA UFUMBUZI KATIKA KIPINJDI CHA SIKU 10: WAZIRI DKT.KALEMANI






Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, na kulia ni Kamu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.

 NA K-VIS BLOG/Mtwara.

Serikali imewaomba wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuwa na subira, katika kipind hiki ambapo upatikanaji wa umeme kwenye mikoa hiyo umeathirika baada ya mashine 5 kati ya 9 za kufua umeme (turbines) kuharibika.

Hata hivyo Mafundui wa TANESCO wamekuwa katika juhudi kubwa za kuzifanyia matengenezo mashine hizo, zilizofungwa miaka 10 iliyopita.

"tayari tumeagiza vipuri kwa ajili ya kutengeneza mashine hizo ambazo kwa ujumla wake huzalisha Megawati 18 za umeme, ambazo zitawasili ndani ya siku 7 ili kuweza kuondoa tatizo la kuzimika umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara." Alisema Dkt. Kalemani.

Alisema, baada ya kwasili kwa vipuri hivyo, kazi ya kuzifanyia matengenezo itaendelea na amememuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, kuleta wataalamu wote wa TANESCO popote walipo nchini, wafika Mtwara na kuungana na wataalamu waliopo ili kazi ya kuzitengeneza mashine hizo iende kwa kasi.

Kati ya mshine 9 ni mashine nne tu zinazotoa Megawati 8 ndio zinafanya kazi, hali inayosababisha kuwepo kwa mgao wa umeme unaofikia hadi masaa 8 kwa siku.

 Dkt. Kalemani ambaye amewasili mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea juhudi za Mafundi wa TANESCO  za kurejesha upatikanaji wa umeme katika hali yake ya kawaida amesema vipuri hivyo vifungwe kwa muda wa siku tatu badala ya wiki 3na kwamba ndani ya siku 10 umeme utakuwa katika hali yake ya kawaida.

Mkoa wa Mtawara na Lindi unategemea mashine hizo zinazozalisha umeme unaotumia gesi asilia.
Ukiachilia mbali kuharibika kwa mashine hizo, miundombinu mingine ya umeme kwenye mikoa hiyo iko salama na katika ubora wa hali ya juu ambapo vituo vipya vya kupoza na kusambaza umeme wa 132kV hapo hapo mkoani Mtwara na kingine huko Mahumbika mkoani Lindi vinafanya kazi pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme (transmission lines), nao uko katika hali bora.


 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Evod Mmanda, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt,. Tito Mwinuka, wakitembelea kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medardi Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika
 Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
  Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
 Fundi wa TANESCO, akichukua spana ili kuendelea na kazi.
 Hii ni moja kati ya mashine zizlizoharibika.

No comments:

Post a Comment