Monday, October 16, 2017

Tanzania kuwakilishwa na timu mbili katika mashindano ya Cana kanda ya tatu ya kuogelea Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Hilal Hemed Hilal akishindana wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea. Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Collins Saliboko akichuana katika mashindano ya Taifa ya kuogelea. Dar es Salaam. Tanzania itawakilishwa na timu mbili za kuogelea katika michezo ya kanda ya tatu ya kuogelaa ya Afrika yaliyopangwa kuanza Alhamis katika bwawa la Hopac la jijini. Tanzania imepewa nafasi ya kuwa na timu mbili kutokana na kuwa mwenyeji.Katibu Mkuu wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka alisema jana kuwa timu ya kwanza imepewa jina la Tanzanite ambayo itakuwa na jumla ya wachezaji 30 na ya pili inajulikana kwa jina la Platinum ambayo itakuwa na wachezaji 21. Namkoveka alisema kuwa timu ya Tanzanite itakuwa na wachezaji 15 wanaume na 15 wanawake na ile ya Platinum itakuwa na wachezaji tisa wanawake na 12 wavulana.Timu hizo zipo kambini hotel ya Giraffe chini ya makocha, Alexander Mwaipasi na Michel Livingstone na zinafanya mazoezi yake kwenye bwawa la Hopac kila siku. Wachezaji wanaoumda timu ya Tanzanite ni Rania Karume , Chichi Zengeni, Maia Tumiotto, Smriti Gokarn (Sonia Tumiotto, Anjani Taylor ambao wote wanatoka klabu ya DSC, huku wengine ni Natalie Abwooli Sanford (MIS), Anna Guild, Emma Imhoff (MSC), Sanne Kleinveld ( ISM Moshi), Angelica Spence, Tara Behnsen, Tami Triller,Kayla Gouws na Amani Doggart ambao wanatoka klabu ya Taliss. Wachezaji wanaume ni Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb O’Sullivan, Khaleed Ladha na Matthew Guild wanatoka klabu ya Mwanza, Chris Fitzpatrick (ISM Moshi), Marin DE Villard (DSC), Adil Bharmal, Hilal Hilal, Harry McIntosh, Dhashrrad Magesvaran (Taliss) na wanaotoka klabu ya shule ya kimataifa ya Morogoro ni Joseph Sumari, Collins Saliboko na Dennis Mhini. Wachezaji wanaounda klabu ya Platinum kwa upande wa wanawake ni Shivan Bhatt, Natalia (Taliss), Charlotte Sanford, Vanessa Dickson (MIS), Rebecca Guild, Meredith Boo (MSC), Maria Bachmann ( ISM Moshi), Kayla Temba na Maya Somaiya ambao wote wanatoka klabu ya DSC. Wanaounda timu ya wanaume ni Aravind Raghavendran, Mohameduwais Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa( ISM Moshi), Terry Tarimo, Aliasgar Chakera(Taliss), Zeke Boos (MSC), Yuki Omari, Augustino Lucas (Champion Rise), Fallih Ahmed (Taliss), Carter Helsby (MSC), Ian Lukaza(ISM) na Emmanuel Stenson wa shule ya kimataifa ya Morogoro. Namkoveka alisema kuwa mchezaji Hilal Hilal ambaye yupo kambini Dubai atajiunga na wenzake kesho katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux, Coca Cola, Label Promotions , Print Galore na Slipway Hotel. Mbali ya Tanzania, mashindano hayo pia yatashirikisha waogeleaji kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Sudan na Kenya.


Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Hilal Hemed Hilal akishindana wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea.
Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Collins Saliboko akichuana katika mashindano ya Taifa ya kuogelea.



Dar es Salaam. Tanzania itawakilishwa na timu mbili za kuogelea katika michezo ya kanda ya tatu ya kuogelaa ya Afrika yaliyopangwa kuanza Alhamis katika bwawa la Hopac la jijini.

Tanzania imepewa nafasi ya kuwa na timu mbili kutokana na kuwa mwenyeji.Katibu Mkuu wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka alisema jana kuwa timu ya kwanza imepewa jina la Tanzanite ambayo itakuwa na jumla ya wachezaji 30 na ya pili inajulikana kwa jina la Platinum ambayo itakuwa na wachezaji 21.

Namkoveka alisema kuwa timu ya Tanzanite itakuwa na wachezaji 15 wanaume na 15 wanawake na ile ya Platinum itakuwa na wachezaji tisa wanawake na 12 wavulana.Timu hizo zipo kambini hotel ya Giraffe chini ya makocha, Alexander Mwaipasi na Michel Livingstone na zinafanya mazoezi yake kwenye bwawa la Hopac kila siku.

Wachezaji wanaoumda timu ya Tanzanite ni Rania Karume , Chichi Zengeni, Maia Tumiotto, Smriti Gokarn (Sonia Tumiotto, Anjani Taylor ambao wote wanatoka klabu ya DSC, huku wengine ni Natalie Abwooli Sanford (MIS), Anna Guild, Emma Imhoff (MSC), Sanne Kleinveld ( ISM Moshi), Angelica Spence, Tara Behnsen, Tami Triller,Kayla Gouws na Amani Doggart ambao wanatoka klabu ya Taliss.

Wachezaji wanaume ni Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb O’Sullivan, Khaleed Ladha na Matthew Guild wanatoka klabu ya Mwanza, Chris Fitzpatrick (ISM Moshi), Marin DE Villard (DSC), Adil Bharmal, Hilal Hilal, Harry McIntosh, Dhashrrad Magesvaran (Taliss) na wanaotoka klabu ya shule ya kimataifa ya Morogoro ni Joseph Sumari, Collins Saliboko na Dennis Mhini.

Wachezaji wanaounda klabu ya Platinum kwa upande wa wanawake ni Shivan Bhatt, Natalia (Taliss), Charlotte Sanford, Vanessa Dickson (MIS), Rebecca Guild, Meredith Boo (MSC), Maria Bachmann ( ISM Moshi), Kayla Temba na Maya Somaiya ambao wote wanatoka klabu ya DSC.

Wanaounda timu ya wanaume ni Aravind Raghavendran, Mohameduwais Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa( ISM Moshi), Terry Tarimo, Aliasgar Chakera(Taliss), Zeke Boos (MSC), Yuki Omari, Augustino Lucas (Champion Rise), Fallih Ahmed (Taliss), Carter Helsby (MSC), Ian Lukaza(ISM) na Emmanuel Stenson wa shule ya kimataifa ya Morogoro.

Namkoveka alisema kuwa mchezaji Hilal Hilal ambaye yupo kambini Dubai atajiunga na wenzake kesho katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux, Coca Cola, Label Promotions , Print Galore na Slipway Hotel.


Mbali ya Tanzania, mashindano hayo pia yatashirikisha waogeleaji kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Sudan na Kenya.

No comments:

Post a Comment