Thursday, October 30, 2014

AJALI MBAYA YA HIACE NA ROLI ILIYOTOKEA JANA ARUSHA YAUWA 13: YUMO JAJI, PROFESA, OFISA ELIMU WA HALMASHAURI.


Ajali mbaya imetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni huko maeneo ya Madira Arumeru jijini Arusha, iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace na Roli lenye tera. Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hiace iliyokuwa ikijaribu kuovatake eneo lisilo salama. Katika ajali hiyo watu kadhaa wamepoteza maisha hususan waliokuwa katika Hiace.
WATU 13 akiwamo mke wa Jaji, Profesa John Luhangisa, Retisia Luhangisa ambaye ni Ofisa Elimu wa Taaluma wa Halmashauri ya Meru mkoani hapa, wamefariki duniani baada ya gari la abiria aina ya Hiace walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.

Katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru maelfu walifurika kwa ajili ya kutambua jamaa zao ambapo mke na mume ambao ni Elly Kaaya, Ofisa Elimu na Kumbukumbu wa Halmashauri ya Meru na mumewe Kundaeli Kaaya ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Ndoombo wilayani Arumeru walikuwa ni miongoni mwa maiti zilizotambulika katika ajali hiyo.
Tukio hiilo limetokea jana eneo la Madila kwenye Kijiji cha Sing’isi saa 11 jioni baada ya gari hilo la abiria lililokuwa linatokea Usa River kwenda Arusha kugongana na lori hilo lililokuwa linatoka Arusha kwenda Kilimanjaro.
Wengine waliotambuliwa katika ajali hiyo ni pamoja na Ofisa Elimu wa Taaluma Halmashauri ya Meru, Zakia Katunga na kondakta wa gari hilo, Simon Wilenya na abiria Kundaeli Kadoya.
Hadi jana jioni, miili mingine sita ilikuwa bado haijatambulika, huku mamia ya watu wakiendelea kufika katika uwanja wa chumba cha kuhifadhi maiti kutambua miili hiyo.
Hata hivyo, hadi jana dereva wa gari la abiria alikuwa hajulikana alipo na majeruhi wengine watatu walikuwa wamelazwa wakiwa mahututi Hospitali ya Wilaya ya Meru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kesho (leo) angetoa taarifa ya tukio hilo.
Jaji Luhangisa aliteuliwa hivi karibuni, kuwa Jaji na Rais Jakaya Kikwete.
Kabla ya uteuzi huo, alikuwa msajili wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Hiace hiyo kwa  upande wa mbele.
Polisi wa usalama barabarani wakisimamia zoezi la kuiondosha Hiace hiyo kwenda kuhifadhi mahali stahili.
Roli hilo lililogongana na Hiace 

'Nyanganyanga' hali ilikuwa si shwari...
PICHA KWA MSAADA WA MITANDAO.

No comments:

Post a Comment