Sunday, October 14, 2012

MKUU WA MKOA WAMWANZA AFUNGUKA ZAIDI JUU YA KIFO CHA KAMANDA WA POLISI MWANZA






Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa mwanza EVARIST NDIKILO amesema kuwa uchunguzi dhidi ya mauaji ya KAMANDA BARLOW tayari umeanza na kwamba polisi inamshikilia mwalimu DOROTHY MOSES ambaye alikuwa akipelekwa nyumbani  na kamanda huyo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza LIBERATUS BARLOW ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia jumamosi oktoba 13 mwaka huu katika eneo la kitangiri manispaa ya ilemela mkoani Mwanza.


Hili ndilo geti ambalo kifo cha Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Barlow kilitokea usiku wa kuamkia leo wakati mwalimu Dorcas Moses alipokuwa akirudishwa nyumbani kupitia lifti ya Kamanda Barlow.

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa inasema kuwa Kamanda Barlow alikuwa akitokea kwenye kikao cha Harusi ya ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto kilichokuwa kikifanyika katika Hoteli ya Florida na kisha akampa lifti mwanamke aitwaye Dorcas Moses ambaye ni mwalimu ya  msingi Nyamagana maeneo ya barabara ya kona ya Bwiru kuelekea Kitangili.

Walipofika getini kwa Dorcas walijitokeza watu wawili waliokuwa wamevaa makoti ya Polisi Jamii, mama Dorcas akamwuliza Kamanda kama anawafahamu watu hao, naye bila shaka akasema kuwa hao ni vijana wa ulinzi jamii wako doria.

Sekunde chache baadaye vijana hao wakaongezeka na kuwa sita wakaanza kuzozana huku kamanda huyo akiwauliza kwani hamnijui mimi ni nani, wakiendelea kumtilia ngumu kutomfahamu na watu hao wakizidi kulizingira gari lake marehemu, kamanda Barlow akajaribu kuchukuwa radio call kuwasiliana na askari wake. 

Jamaa hao hawakumruhusu kamanda afanye mawasiliano kwani papo hapo walimfyatulia risasi kichwani iliyopelekea kifo chake.  

 Mwili wa marehemu LIBERATUS BARLOW umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kusubiri taratibu za mazishi.

No comments:

Post a Comment