Mkuu wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo
………………………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Erick Mwarabu(37) mkazi wa Kitongoji cha Kazamoyo wilayani Rufiji ,mkoani Pwani ,ameuawa kwa kupigwa risasi mbili za ubavuni na moja ya kichwani .
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo ,wameeleza marehemu ameuawa usiku wa kuamkia June 6 mwaka huu ikiwa ni siku mbili toka mwenge wa Uhuru utoke wilayani hapo .
Rukia Zuberi na Ajabu Mussa wamesema ,watu wanaodhania ni wauaji walivunja mlango wa nyumba yake saa 9.00 usiku kisha kuingia ndani na kutekeleza mauaji hayo.
Aidha wamesema ,marehemu alijificha uvunguni baada ya kusikia mlango unavunjwa na mkewe kuulizwa kama yeye yupo hivyo kuamua kujificha uvungu wa kitanda .
Mussa ameeleza ,wauaji walimtafuta ambapo walimuona kisha kumpiga risasi tatu .
Nae mganga mfawidhi katika Kituo cha afya Ikwiriri ,Dk.Iddi Malinda ,amekiri kupokea tukio hilo .
Amesema uchunguzi umebaini marehemu amepigwa risasi ya kichwani na mbili ubavuni ambapo mwili wake umekabidhiwa kwa ndugu .
Jeshi la polisi mkoani Pwani ,linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo .
Kwa upande wake ,mkuu wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo ,amesema bado vyombo vya usalama vinajiridhisha na upepelezi .
No comments:
Post a Comment