Mtandao wa kijamii wa Facebook
utaanza kuuza hisa zake baadaye kwenye soko la hisa la New York, katika
mkupuo mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa wa uuzaji wa hisa katika miaka ya
hivi karibuni.
Mwasisi wa mtandao huo, Mark Zuckerberg
alifungua biashara katika soko la hisa la Nasdaq ingawa hisa za Facebook
hazitauzwa hadi baadaye.Hisa za kampuni hizo ziligonga thamani ya zaidi ya dola bilioni moja.
Mkupuo wa kwanza uliotolewa, ambao ni mkubwa kuwahi kutolewa, uliingiza zaidi ya dola bilioni 18 kwa mtandao wa Facebook na wanahisa wake waliopo katika biashara.
Tangu kuanzishwa kwake, miaka nane iliyopita, Facebook ni moja ya kampuni zenye teknolojia ya thamani ya hali ya juu miongoni mw kampuni za mitandao ya kijamii. Kampuni hiyo ina watumiaji wa kila mara wa huduma zake wapatao milioni mia tisa.
Mark Zuckerberg alionekana kupitia video katika makao makuu ya kampuni hiyo wakisherehekea mjini California.
Bei ya hisa moja ni dola 38.
No comments:
Post a Comment