Afisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael, akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 30 Mkurugenzi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Efesper
|
Afisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada wa shilingi milioni 30 kwa Mpangwa Taifa. |
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiudhuria press conference.
Kampuni ya Tigo Tanzania, kwa mara nyingine tena imehaidi kuunga mkono suala muhimu la maadhimisho ya siku ya uchangiaji
damu kwenye siku ya dunia ya wachangiaji damu yatakayofanyika mkoani Mara
tarehe 14 Juni, 2013. Zoezi hili lakuchangia damu yatafanyika katika mikoa yote
hapa nchini yetu ambapo uzinduzi wa
mpango hu wa taifa hutafanyika mkoani
mara kitaifa zitafanyika mkoani Mara
nakuendelea katika mikoa mengine hapa nchini.
“Huduma ya kuchangia damu kwa mara nyingine
imevutia kufanyiwa kazi na Tigo katika juhudi za kuinua uelewa wa jamii juu ya
umuhimu wa kujitolea kuchangia damu katika kuhakikisha upatikanaji wa damu
salama na ya kutosha. Zoezi hili la uchangiaji wa damu litarajia kupunguza, kwa
kiasi kikubwa, uhaba wa damu uliopo hivi sasa unaozikabili hospitali nyingi
nchini, na kwa maana hiyo kuwezesha kuzuia vifo visivyo vya lazima, hususa, kwa
wanawake na watoto ambao ndio wahitaji wakuu wa damu…. Ningependa kuchukua
fursa hii kuishukuru kampuni ya Tigo kwa msaada wake imara kwenye mpango huu
unaolenga kuwapatia Watanzania maisha bora na yenye afya”. Alisema Dk. Efesper A. Nkya, program meneja wa
mpango wa NBTS
Afisa Mahusiano ya Jamii na Matukio
wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ,
Woinde Shisael alisema; “Kampuni ya Tigo
inajisikia fahari kwa kuwemo kwake katika mpango huu wenye lengo la
kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu salama, huku tukiwashukuru
wachangiaji damu waliopo na pia kutoa wito kwa wachangiaji wapya kujitokeza
kuchangia damu. Afya ya jamii ni muhimu sana kwa kampuni ya Tigo na hivyo
kuifanya Tigo kujihususha kikamilifu katika mpango huu. Hili ni jambo
linalohitaji msaada wa kila mmoja wetu”.
Shisael aliongeza kusema kwamba; “ Napenda kuchukua
fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuipa
muhimu unaostahili suala hili na kujitokeza kuchangia damu na hivyo kuokoa
maisha ya wahitaji kama kaulimbiu ya mwaka 2013 inavyosema “Kila mchango wa Damu ni zawadi kwa maisha”. Tigo itaendelea
kushirikiana na kuwekeza katika sekta ya afya nchini kwajili yakuhakikisha kwamba Watanzania wote wanaendelea kua na afya nzuri.
Siku ya uchangiaji damu duniani ni mpango
uliobuniwa ili kuelimisha kuhusu umuhimu wa damu salama, kuhamasisha uchangiaji
damu wa hiyari na pia kuwashukuru wachangiaji damu bila malipo kwa
mchango wao mkubwa katika kuokoa maisha. Kaulimbiu ya kampeni ya dunia ya
uchangiaji damu 2013 inasema “Kila mchango wa Damu nikama zawadi wa maisha kwa binadam”.
Kuhusu Huduma
ya kutoa Damu ya Taifa
NBTS ilianzishwa
mwaka 2004 na ni mpango chini ya Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii
(MoHSW) na mamlaka ya kuhakikisha upatikanaji wa damu salama ya kutosha kupitia
serikali kuu ni uratibu wa huduma ya kuongezewa damu
nchin Tanzania
Ni ya malengo makuu ni:
1. Kuongeza uwezo wa kukusanya,
usindikaji na kusambazaji wa kutosha wa damu salama na damu kutoka kwa
wafadhili wa hiari ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa.
2. Ili kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kutosha na kupatikana ya damu
salama kutoka kwa wafadhili wa
damu kutokana na idadi ya watu ndani
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Kuanzisha ufuatiliaji na tathmini ya mfumo wa kudumisha ubora, na ufanisi wa
Huduma ya Damu ya Taifa.
NBTS inafanya kazi
nchi nzima na JWTZ na TRCs kama washirika wake kupitia vituo vyake sita ambavyo
ni Kanda ya Dar es Salaam, Mwanza,
Tabora, Mtwara, Mbeya na Moshi.
Kama mdau TACAIDS wamechangia sana katika kuzuia VVU / Ukimwi, tangu kuanzishwa
kwake, na kupunguza kwa kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU, na ni miongoni
mwa wafadhili damu kutoka% 7-10 mwaka 2004 hadi 1.2% katika 2012.
KUHUSU
TIGO:
Tigo
ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka
1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)
Tanzania
bara na visiwani.
Lengo
la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania
kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti
za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha
za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
International
Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko
13 barani
Afrika
na Amerika ya Kusini.
"Tabasamu
upo na Tigo"
|
No comments:
Post a Comment