Mpatanishi wa Mgogoro wa Syria Kofi Annan
Baraza la Kitaifa la upinzani nchini Syria limeutaka Umoja wa
Mataifa kuitisha kikao cha dharura kujadili mauaji ya takriban watu 90
yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya serikali katika mji wa Houla Ijumaa
(25.06.2012).
Mauaji hayo yanakuja wakati Kofi Annan mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Waarabu kwa Syria ambaye alisimamia makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi uliopita yaliokiukwa mara kadhaa,akikamilisha mipango ya kurudi tena Damascus.
Kituo hicho cha Haki za Binaadamu chenye makao yake mjini London Uingereza kimesema kwamba mashambulizi hayo ya mizinga yameuwa zaidi ya watu 90 wakiwemo watoto 25 huko Houla.Shirika hilo limeishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kukaa kimya wakati utawala wa Syria ukifanya mauaji hayo.
Mikanda ya video iliowekwa kwenye mtandao wa You Tube imeonyesha taswira ya kutisha ya maiti za watoto zilizolala sakafuni baadhi ya maiti hizo zikiwa zimepasuka vibaya na sehemu ya kichwa cha mtoto mmoja kikiwa kimeripuliwa.
Awali msemaji wa kike wa Baraza la Kitaifa la upinzani wa Syria Basma Kodmani alisema zaidi ya watu 110 waliuwawa na vikosi vya serikali ya Syria na nusu yao wakiwa ni watoto. Amesema baadhi ya wahanga waliripuliwa na mizinga na kuna baadhi ya familia nzima zilizoangamizwa.
Timu ya waangalizi wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa walioko nchini Syria wamekwenda katika mji wa Houla kutathmini hali hiyo.Timu hiyo imewasili katika kijiji cha Taldau kilioko ukingoni mwa mji wa Houla kushuhudia uhalifu uliotendeka katika kipindi cha saa 24 ukiwa ni ukiukaji wa usitishaji wa mapigano.
No comments:
Post a Comment