Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa ameonya kutokea vita vya
wenyewe kwa wenyewe Syria baada ya wachunguzi hao kuhesabu miili 92, 32
ikiwa ni ya watoto ,katikati ya mji wa Houla kufuatia ripoti
za mauaji.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amejiunga na sauti
za kimataifa kushutumu mauaji hayo siku ya Jumamosi , huku
kukiwa na miito kwa dunia kuchukua hatua kusitisha umwagikaji wa
damu.
mjumbe wa UN na Arab league nchini Syria Kofi Annan
Jeshi la waasi la Free Syria, Syria huru , FSA, limesema
halifuati tena mpango unaoungwa mkono na umoja wa mataifa nchini
Syria hadi pale kutakapokuwa na uingilia kati wa umoja wa
mataifa kuzuwia mauaji ya raia, na kutoa wito wa mashambulio ya
anga dhidi ya majeshi ya serikali.Vita vya wenyewe kwa wenyewe
Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa meja jenerali Robert Mood amekiita kile kilichotokea mjini Houla , kuwa maafa ya kinyama. Wachunguzi wa kiraia na kijeshi wa Umoja wa mataifa walikwenda mjini Houla na kuhesabu miili 32 ya watoto na zaidi ya 60 ya watu wazima waliouwawa, Mood amewaambia waandishi habari mjini Damascus siku ya Jumamosi.
Meja jenerali Robert Mood
Kundi linalochunguza hali nchini Syria limesema kuwa watu 114
wameuwawa katika mji wa Houla. Yeyote alieanzisha, yeyote
anayehusika na yeyote aliyefanya vitendo hivyo vya kuchukiza
anapaswa kuwajibishwa, amesema Mood.Wale wanaotumia nguvu kwa ajili ya kutimiza ajenda zao wataleta hali ya kutokuwa thabiti zaidi, hali ambayo haitabiriki na huenda ikaelekeza nchi hiyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ameongeka mkuu huyo wa ujumbe wa umoja wa mataifa.
Ban Ki-moon na Kofi Annan ambaye ni mjumbe wa umoja wa mataifa na mataifa ya umoja wa mataifa ya kiarabu , Arab League, ambaye amekuwa mpatanishi wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo yamekuwa yakikiukwa kila siku tangu yalipoanza kufanyakazi Aprili 12, wamesema kuwa mauaji hayo ya kinyama yanakiuka sheria za kimataifa.
Uhalifu huu wa kinyama na unaochukiza , uliowahusisha matumizi bila kujali na ya kupita kiasi ya nguvu , ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, msemaji wa umoja wa mataifa amemnukuu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon akisema.
No comments:
Post a Comment