MTOTO mwenye umri wa miaka minne, Hassan Ibrahim, mkazi wa Mburahati
amekufa papo hapo baada ya kunaswa na umeme akiwa kwenye sherehe ya
harusi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mtoto huyo alinaswa juzi saa 4.30 usiku katika eneo la Manzese ambapo ilifanyika harusi hiyo.
Alisema kuwa mtoto huyo alinaswa na umeme baada ya kukanyaga waya uliounganishwa na spika ya muziki katika sherehe hiyo ambapo alikufa papo hapo.
Kenyela alisema kuwa maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea na upelelezi zaidi wa tukio hilo.
Wakati huo huo, Mwalimu wa Shule ya Msingi Magomeni, Winnie Bandakele (50), amekufa papo hapo baada ya pikipiki aina ya Bajaji aliyokuwa amepanda kugongwa na gari.
Kamanda Kenyela alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 8 mchana katika barabara ya Wazo Hill eneo la Bondeni na kuhusisha gari lenye namba za usajili T 119 AFS Mitsubish Fusso lililokuwa likiendeshwa na Jeremia Raphael akitokea Wazo kwenda Tegeta.
Wakati dereva huyo akishuka mlima wa Wazo Hill akiwa na gari hilo lilimshinda kushika breki na kugonga gari namba T 862 BED Toyota Carina pamoja na pikipiki mbili ikiwemo bajaji hiyo yenye namba za usajili T 639 BTL iliyokuwa ikiendeshwa na Salum Mkape (23).
Aidha alisema abiria saba waliokuwa kwenye Carina na Bajaji walipata majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao, ambapo watano kati yao walitibiwa na kuruhusiwa na Ramadhan Hussein(30), mkazi wa Wazo Hill pamoja na Salum Mkape wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

No comments:
Post a Comment