Wednesday, June 27, 2012

Assad atangaza hali ya vita Syria

Rais wa Syria, Bashar al- Assad, ametangaza kuwa nchi yake iko katika hali ya vita baada ya miezi 15 ya machafuko yanayoendelea nchini humo.
 Akizugumza wakati wa kuapishwa kwa baraza jipya la mawaziri jana, Assad aliitaka serikali itumie uwezo ilionao kupata ushindi katika mzozo huo. Katika nchi jirani ya Uturuki, waziri mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, ametishia kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Syria iwapo vikosi vya taifa hilo vitaukaribia mpaka wa Uturuki.

Onyo hilo limetolewa baada ya Syria kuidungua ndege ya kivita ya Uturuki Ijumaa iliyopita. Uturuki inadai ndege hiyo ilikuwa katika anga ya kimataifa upande wa bahari ya Mediterenia, huku Syria ikisisitiza kwamba ilikuwa katika anga yake bila idhini.
 Jumuiya ya kujihami ya NATO imeilaani Syria kwa kuidungua ndege hiyo na kuthibitisha tena mshikamano wake na Uturuki.

No comments:

Post a Comment